Na Wounded Shizza,Michuzi Tv -Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta amewataka wadau wa maji katika
Mkoa wa Arusha kuweka wazi taarifa zao za kiutendaji ili kutoa nafasi ya
utatuzi wa changamoto kwa urahisi.
Ameyasema
hayo alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maji wa Mkoa wa Arusha,
kikao hicho kilichojumuisha sekta za umma na binafsi.
Kimanta
amesema uwazi wa taarifa utarahisisha kila mdau kuwa na uwelewa wa
pamoja wa kila sehemu na kurahisha kupata suluhu ya changamoto.
Amesema
mpaka sasa hali ya upatikanaji maji katika Mkoa wa Arusha hasa vijijini
bado ipo chini sana kwani Mkoa ulijiwekea malengo ya kusambaza maji
vijijini kwa 85% ifikapo 2020, lakini mpaka sasa ni 69.5% ya upatikanaji
wa maji vijijini ndio umetekelezwa kuanzia 2015-2020.
Vijiji
304 ndivyo vimeshapata maji hadi kufikia mwaka 2020 na vijiji 86 bado
havijapatiwa maji kati ya vijiji 390 vyote na serikali inaendelea
kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo.
Kimanta
amesema bado malengo ya serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 Mkoa
wa Arusha uwe umefikia 100% ya upatikanaji maji vijijini.
Amesisitiza
kuwa matatizo ya maji niya kila mmoja hivyo amewataka wadau hao
kuhakikisha wanatoka na mpango mkakati mkubwa wa kuwezesha wananchi
kupata maji kwa haraka zaidi.
Akitoa
taarifa ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Arusha Meneja wa wakala wa
maji na usafi wa Mazingira Vijijini injinia Emmanuel Makaidi amesema,
RUWASA imependekeza bajeti ya Bilioni 17 kwa mwaka 2020/2021 na mpaka
Februari 2021 bilioni 7.4 sawa na 58.7% zimeshatumika.
Makaidi
amesema mpaka sasa RUWASA Mkoa wa Arusha imeshatekeleza miradi 4 yenye
thamani ya bilioni 4.6 na miradi 8 inatarajiwa kuanzishwa katika
halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Akitoa
neno katika kikao hicho mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa
Arusha bwana Zeloth Steven amesema ni vizuri sheria ya maji ikafahamika
kwa mapana na kina kwa wananchi ili kuwaongezea uwelewa.
Aidha
amewataka wadau hao wa maji kuhakikisha wana simamia miradi yote ya
maji kwa umakini sana kwani katika kampeni za mwaka 2020 kero kubwa kwa
wananchi ilikuwa ni upatikanaji wa maji katika maeneo mengi.
RUWASA
Mkoa wa Arusha umefanya kikao chake cha kwanza cha wadau kwa lengo la
kujitambulisha kwa wadau na kuweza kushirikiana katika mambo mbalimbali
na wadau hao na kuweza kutatua changamoto zinazowakabili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...