* Wanaounda makundi ya kupotosha katika mitandao ya kijamii kukiona cha moto
*Ni kutokana na uzushi wa taarifa zinazolenga kuweka taharuki jamii
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv- Katavi
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amewataka watanzania kutumia mawasiliano kwa ajili ya maendeleo.
Naibu Waziri ameyasema hayo mjini Mpanda mkoani Katavi kutokana na baadhi ya watu wa kuwa wasemaji katika mitandao wakati Msemaji wa Serikali yupo ambaye anaweza kuzungumzia masuala yeyote yanayoendelea nchini.
Kufuatia na kutumika mitandao vibaya Naibu Waziri amesema mikakati ya kuwabaini wanaopotosha kwenye mitandao ya jamii huku akitaka wanaounda makundi kujiandaa hatua zitakazochukuliwa.
Amesema kuna watu katika mitandao ya jamii wamekuwa sehemu ya kuzusha vitu na kutaka watanzania kuvipuuzia.
Amesema kama suala la ugonjwa wizara afya ipo na ndio wanaweza kuzungumzia ugonjwa.
Amesema mitandao ya kijamii ipo kwa ajili ya kutumika katika maendeleo na sio kuweka taharuki kwa watanzania kwa vitu visivyo na maendeleo.
Amesema mifumo hiyo ikishawekwa Jeshi la Polisi kupitia kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI) watapewa taarifa na hakuna kwa sehemu ya kukimbilia.
Amesema serikali imejenga miundombinu ya mawasiliano katika kuhakikisha wananchi wanapashana habari na sio kufanya watu kufanya vitu ambavyo vinahatarisha jamii.
Naibu Waziri Kundo amesema kuwa watatimiza malengo ya Mh. Rais Dkt.John Magufuli katika kuhakikisha wanasimamia mawasiliano kwa kuleta tija.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...