NA FARIDA SAID MOROGORO.
Kuelekea
Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini
Abdal aziz Abood amekutana na watoto yatima, wazee wasiojiweza pamoja na
watu wenye ulemavu walio chini ya taasisi ya Ukumbusho wa Zaka Tanzania
yenye makao makuu yake Mkoani Morogoro na kuahidi kusaidia futari
katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhan.
Mhe,
ABOOD amekutana na makundi hayo katika Kongamano la kukaribisha mwezi
mtukufu wa Ramadhan lililo andaliwa na Taasisi ya kiraia ya Ukumbusho wa
Zaka Tanzania, inayowasaidia watu wenye mahitaji mbalimbli, wakiwemo
watoto yatima,Watu wenyeulemavu pamoja na wazee wasio jiweza.
Akizungumza
katika kongamano hilo Mhe Abood amesema pamoja na kuchangia futari
katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini pia atatoa
mavazi kwa vijana 80 wanalelewa na taasisi hiyo katika siku kuu ya EDD
ELFITRI ili wawezi kufurahia sikuku hiyo kama vijana wengine.
“Mimi
kama Mbunge wenu nawapatia mavazi ya kusherekea siku kuu ya Edd watoto
wote yatima ambao nimeambia idadi yao ni 80 waliopo hapa kwenye jumuiya
ya Ukumbusho wa Zaka Tanzania na nitaendelea kushirikiana nanyi kwa
kila jambo.”Alisema Mhe Abood.
Wakati
huo huo Mhe Abood amekabidhi kitimwendo kwa taasisi ya Ukumbusho wa
Zaka kitakacho wasaidia watoto wenye ulemavu wanao lelewa na taasisi
hiyo, ambao awali walikuwa na uhitaji wa kiti hicho kinacho wasaidia
kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
“Kutoa
msaada kwa watu wasio jiweza ni moja ya njia ya kupata thawabu, lakini
pia kunasaidia kudumisha upendo kwa ndugu na jamaa zetu, na ndio maana
hata kwenye Quaran tukufu na vitabu vingine vya dini vimeandika na
mwenyezi mungu ametuamrisha kuwasaidia watoto yatima na watu wasio na
uwezo.”Alisema Mhe Abood.
Awali akiwasilisha
changamoto zinazo wakabili katika jumuiya hiyo kwa Mbunge wa jimbo la
Morogoro Mjini Mhe Abdalaziz Abood ,Mwenyekiti wa Jumuiya Sheikh Omari
Mahmudu Katura amemuomba Mhe ABOOD awasaidie kuwatafutia wahisani
watakao weza kuwasaidia makundi hayo ya watu wenye uhitaji .
Pia
wamewataka watanzaia kutoa misaada katika vituo maalumu vya kulelea
watoto yatima na watu wasiojiweza, kwani kufanya hivyo kutasidia kufikia
kundi kubwa zaidi kuliko kutoa kwa mtu mmoj mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...