Na Khadija Seif, Michuzi Tv.
MSANII Wa Bongomovie Salim maarufu Kama Gabozigamba asherehekea 40 ya Mtoto wake na Mastaa mbalimbali.
Mastaa hao ambao wamehudhuria kwenye hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa holiday inn jijini Dar es salaam ni pamoja na Alikiba,Barnaba,Dulla Makabila,Mkali wenu ,Idris sultan ,Shilole ,Lamata na wengine wengi.
Katika hali ya kushangaza,Mkali wenu kutoka kiwanda cha uchekeshaji amevunja mbavu watu ukumbini baada ya Mshereheshaji dk.Kumbuka kumuita kutoa zawadi kwa mtoto.
"Sikupewa taarifa hiyo awali Nina nauli tu elfu 10 hivyo nitaitoa Kama zawadi ,usafiri Nitaomba lift kwa Alikiba ."
Wengine walioweza kutoa zawadi ni pamoja na Alikiba ,Dulla Makabila na wengine ambao wameweza kuhudhuria shughuli hiyo.
Pia kwa upande Mwengine Idris sultan amempongeza Gabozigamba na kumtakia afya njema mtoto wake Bills na kusema mbali na kazi za Sanaa anaijua dini vizuri na amefuzu juzuu 30 .
"Nimelelewa na Mama pamoja na baba yangu ambae anaijua Misingi ya dini kwani ni imamu hivyo najivunia Hilo."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...