Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
Timu
ya Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kutoka katika baadhi ya vyuo
,wametembelea mradi mkubwa wa bwawa la kufua umeme la mwalimu Nyerere
liliko Rufiji mkoani Pwani ,ili kujifunza na kujionea kazi iliyofanywa
na serikali awamu ya tano kipindi cha Hayati Rais Dkt. JOHN POMBE
MAGUFULI.
Akizungumza
mara baada kutembelea mradi huo , Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo
kikuu cha sayansi na teknolojia cha Mbeya HILARY LOOKEN ambao ndio
walioandaa ziara hiyo, anasema mbali ya kujifunza kivitendo lakini pia
wanasapoti juhudi za serikali awamu ya tano katika kuipeleka Tanzania
katika viwango vikubwa vya kiuchumi kwani mradi huo pamoja na faida
nyingi utaeza kuwanufaisha watanzania katika nyanja mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kuhifadhi mazingira.
"
Tumeona tuje kujifunza katika mradi huu kwani katika chuo chetu tuna
fani mbalimbali zinazotolewa ikiwa ni pamoja na Fani ya uinjinia, hivyo
wanafunzi wamejifunza mengi katika mradi, na niseme tu naipongeza
serikali kwa kufanya mradi huu mkubwa wa kimkakati ambao utakwenda
kutupeleka katika viwango vingine kiuchumi,"
Alisema HILLARY LOOKEN , Rais wa Serikali ya Wanafunzi chuo cha Sayansi sayansi na teknolojia cha Mbeya (MUST).
Mradi
huu unajengwa na mkandarasi wa kampuni ya Arab Contractor kutoka Misri
utagharimu kiasi cha Trilioni 6.5 na unatarajiwa kujengwa kwa kipindi
cha miezi kati ya 36 mpaka 42 ya ukamilishaji wa mradi huo.
Kukamilika
kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi, kutaiwezesha Tanzania kuzalisha
kiasi kikubwa cha umeme kitachokasaidia kutekeleza miradi mikubwa ya
kimkakati ikiwemo ujenzi wa uchumi wa viwanda na mradi wa reli ya
kisasa,.
Mhandisi
DAVID MUNKALA ni Mtaalamu wa Maji wa Mradi wa Julius Nyerere,
alisema Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji
la Julius Nyerere kwenye bonde la mto Rufiji unaendelea kwa kasi
inayohitajika na kuwa unatarajiwa kukamilika kipindi cha mkataba
uliosaniwa.
BAADHI YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KIKIWEMO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
MBEYA (MUST) WAKIMSIKILIZA MHANDISI DAVID MUNKYALA (KATIKATI) AMBAYE NI
MTAALAMU WA MAJI KATIKA MRADI WA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MWALIMU NYERERE
LILILOKO RUFIJI, WAKATI WALIPOTEMBELEA MRADI HUO WA KIMKAKATI
UNATEKELEZWA NA SERIKALI KWA ASILIMIA 100, ILI WAWEZE KUJIFUNZA NA
KUJIONEA MAENDELEO YA MRADI HUO.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...