Nyota watatu wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao waliongia kwenye kinyang’anyiro hicho ni Clatous Chama, Aishi Manula na Shomari Kapombe ambao mmoja wao atashinda kutokana na idadi ya kura atakazopata.

Wachezaji watano waliingia kwenye kinyang’anyiro hicho lakini Kamati maalumu iliwachuja na kubaki na watatu ambao watapigiwa kura na mashabiki kupitia Tovuti rasmi ya klabu. Nyota wawili ambao walifika hatua hiyo ni Luis Miquissone na Pascal Wawa.

Tuzo hii ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile itakuwa ni ya tatu kutolewa tangu ilipoanza mwezi Februari mwaka huu.

Mchezaji atakayepata kura nyingi atakabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium.

Miquissone alikuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mwezi Februari wakati Joash Onyango alishinda mwezi Machi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...