KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dara es Salaam (DCPC), kinampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa.
 
Pia DCPC imefurahishwa na kauli ya Rais Samia kuwataka watendaji wa wizara hizo kuacha kutumia mabavu wakati wa kufanya maamuzi badala yake watumie kanuni na sheria zilizopo.
 
Sisi DCPC tunaamini watendaji wa Wizara ya Habari ya Habari, Sanaa na Utamaduni watayafanyia kazi kwa haraka maagizo ya Rais Samia na kurejesha ajira za wanahabari na wafanyakazi wa idara nyingine zilizopotea kwa kufungwa kwa vyombo vya habari.
 
DCPC tunaamini kwamba sasa uhuru wa vyombo vya habari uliominywa kwa miaka kadhaa sasa unarejea.

Pia tunaiona azma ya Rais Samia ya kuongeza mawanda ya ukusanyaji wa kodi na kusaidia katika kuleta maendeleo ya nchi.
 
Uamuzi huu wa Rais Samia umekuja wakati muafaka kwani tasnia ya habari kwa miaka mitano ilipita kwenye wakati mgumu hali iliyosababisha kundi kubwa la wanahabari mahiri na makini kukosa kazi.

DCPC tunatoa wito kwa wanahabari kuendelea kufanyakazi zao kwa weledi na kuzingatia sheria ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 na kanuni za utangazaji ili kufanyakazi kwa amani kwa kuwa tasnia ya habari ni mhimili wa nne wa dola.


Irene Mark
Mwenyekiti DCPC
06/04/2021




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...