Na Humphrey Shao,Dar es Salaam

DIWANI wa Kata ya Mbezi jijini Dar es Salaam Ismail Malata amesema kuna jumla ya zaidi ya Sh.bilioni 1.2 zimetolewa na wananchi kwa ajili ya maeneo yao kupimwa lakini kampuni ambazo zichukua fedha hizo za wananchi zimeshindwa kupima na kuweka mawe ndani ya kata hiyo.

Malata amesema hayo katika mkutanao wake na wakazi wa Mbezi alipokuwa akijibu moja ya hoja za wananchi ambao waliuliza swali kuhusu nini kinaendelea katika miradi ya upimaji ardhi.

"Nimebaini uozo mkubwa sana katika miradi hii ya upimaji katika mitaa yote Nane kiasi ambacho hakivumiliki kwani fedha zimelipwa na hakuna kinachoonekana na upimaji umesimama wakati fedha zimeshatolewa na wananchi kiasi cha Sh.bilioni 1.2," amesema Malata .

Ameongeza mpaka sasa watu waliopewa hati miliki kutokana na miradi hiyo hawafiki 200 huku ripoti ikionesha watu zaidi ya 3000 wamelipa katika kampuni ya upimaji .

Aidha ameoneshwa kusikitishwa kitendo cha wakazi wa Mbezi kushindwa kulipa mikopo ya halmashauri hali iliyosababisha watu wengine kukosa fursa ya kukopa.

Malata ametoa mwito kwa viongozi wa Vikundi kuwasihi wananchama wao kurejesha fedha hiyo kwani azina riba kama ilvyo fedha za tasisi nyingine.

Hata hivyo Michuzi TV na Michuzi Blog itaendelea kufuatilia suala hilo ili kupata maelezo ya ufafanuzi kutoka kwa wahusika wakiwemo wamiliki wa kampuni ambazo zimelipwa fedha hizo kwa ajili ya kupima.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...