………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amewataka Waandishi wa
Habari nchini kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuepuka makosa ya
kisheria yanayoweza kujitokeza.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo
jijini Dodoma alipokuwa akitoa mada juu ya ”Matumizi ya Mitandao ya
Kijamii”’ wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari za mtandaoni wa
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) (TBConline).
Amewataka kutojiona wanyonge kwa
kufanya kazi hiyo, bali wajione watu waliobeba dhamana kubwa katika
kuihabarisha jamii mambo mbalimbali yanayoendelea duniani.
“Si lazima Waandishi wote wa
Habari waonekane kwenye Televisheni, kuna namna nyingi za kufanya kazi
hii ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo watumiaji wake wanaongezeka kwa
kasi, kwa sasa dunia imehama kutoka mtaani kwenda mtandaoni.”
amefafanua Dkt. Abbasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...