Jane Edward, Michuzi TV, Arusha


WIZARA ya afya imesema itawachukulia hatua watumishi wote wasiokuwa waadilifu ambao wanahusika na wizi wa Vyandarua vyenye dawa vinavyotolewa na wizara hiyo kwa wananchi kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa Maralia.

Waziri wa afya,maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto,Dkt.Doroth Gwajima,ameyasema hayo leo kwenye maadhimisho ya siku ya Maralia dunia yaliyoadhimishwa  kitaifa kwenye viwanja vya Ngareanaro Mkoani Arusha.

Amesema wapo baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu wamekuwa wakihusika na upotevu wa Vyandarua hivyo vyenye dawa ,akamuagiza Mkurugenzi wa kinga wizara ya afya wapelekee orodha ya wezi wa vyandarua ili wizara iwachukulie hatua.

Waziri,Gwajima,amesema wizara  inatekeleza mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa Maralia nchini ambao madhara yake ni makubwa na lengo la wizara ni kuwezesha kuzalisha watoto wenye afya  ambao hawana maambukizi ya maralia

Amesema Wizara itaendelea kusimamia utolewaji wa vyandarua vyenye dawa bure kwa wajawazito na watoyo watato watakaokuwa  wakienda Kiliniki kwa ajili ya kutokomeza Maralia.

Ameipongeza mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara kwa kutokomeza Maralia ambapo kiwango cha maambukizi ni asilimia moja tu, na nguvu  inaelekeza kwenye mikoa ya Geita,Kagera ,Kigoma na Mtwara,ambayo kiwango cha maambukizi ni asilimia 15.

MKUU wa Mkoa wa Arusha,Idd  Kimanta,amesema mikoa ya Arusha,Manyara, Kilimanjaro imefanikiwa kupunguza maambukizi kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kiwango cha maambukizi ni  asilimia moja tu,ambayo wanajipanga kutokomeza kiwango kiwe ni sifuri.

Kwa upande wake kiwanda cha nguo cha Ato Z,kimemkabidhi Waziri  Vyandarua vyenye dawa 1500,ambavyo vitatolewa kwenye mikoa yenye maambukizi.

Mwakilishi wa kiwanda hicho, Sylivesta Kazi,amesema kuwa vyandarua hivyo ni mchango wa kiwanda hicho katika kutokomeza Maralia hapa nchini.

Jofrey Nyamasagi ni afisa maendeleo Tridem Pharma ambao wanashughulika na kuagiza dawa za kutokomeza Malaria hapa nchini,anasema kwa SASA wanajivunia namna ugonjwa huo wa Malaria ulivyopungua hapa nchini tofauti na ilivyokuwa zamani na kama wadau wa wizara ya afya wataendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa wizara hiyo I'll kufikia malengo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...