FOUNDATION  for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na  Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Serikali (TANGO)  pamoja na Shirika la Equality for Growth  (EfG) yamekutanisha wadau mbalimbali kutoka  asasi za kiraia kwa lengo la  kujadili   matakwa ya sheria na miongozo inayosimamia na kuratibu sekta ya Asasi za Kiraia nchini Tanzania baada ya sheria hizo kufanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Mkutano uliofanyika kwa siku mbili,kuanzia Machi 30 hadi Machi 31  Machi mwaka huu kwa njia ya  una mtandao   na kuwakutanisha wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia (AZAKI) mbalimbali nchini na AZAKI zinazowezeshwa na FCS kwa lengo la kutoa elimu juu ya utekelezaji wa Sheria hizo , kuzipitia ili kuona namna ambavyo zitatekelezwa sambamba na kutoa fursa kwa wadau hao kutoa maoni yao.

Akizungumza kuhusu mkutano huo, Meneja Idara ya Kujenga Uwezo  FCS Edna Chilimo amesema mkutano huo uliwakutanisha jumla ya asasi za kiraia 300 ambapo mada mbalimbali zilitolewa  na baadhi ya wataalamu kutoka katika Ofisi ya usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) Usajili wa Jumuiya za Kijamii, na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ikiwa na lengo la kutoa elimu na uelewa mpana kwa Asasi hizo kuhusu maboresho ya Sheria hizo.

“Kuna chanagamoto kubwa katika uelewa na tafsiri ya sheria hizo,  wapo wengine walikuwa hawazielewi na wengine walikuwa na tafsiri potofu, wengine walihamaki hivyo FCS kama mwezeshaji baada ya kugundua tatizo tukashirikiana na wadau wengine.


 "Ambao ni mashirika ya kimtandao ambayo ni  NaCoNGO, TANGO na  EQUALITY FOR GROWTH (EfG)   kutengeneza Programu ya kuwawezesha Asasi za kiraia kuelewa sheria hizo vizuri na wapate tafsiri sahihi ili mwisho wa siku waweze kuzifuata na kuzifanyia kazi ili waweze kutekeleza miradi yao kwa weledi wakiwafikia wananchi na kuhakikisha wanafuata sheria hizo ” amesema Edna.

Aidha amefafanua katika programu hiyo licha ya kutoa elimu ya kuwajengea uwezo wa uelewa wa Sheria hizo pia inalenga  kutoa msaada kwa yale mashirika yaliyokuwa yanahitaji msaada wa kitaalamu  ili waweze kuelewa zaidi ili kila mmoja aweze kufikia malengo.

“Programu hii tunaifanya kwa karibu na watu wa Serikali kwakuwa wao ndio wasimamizi wa hizo sheria hivyo tumefanya kazi na Ofisi ya msajili wa NGOs, Ofisi ya Msajili wa Jumuiya na Ofisi ya Msajili kutoka RITA ambao walipata nafasi nzuri sana ya kufafanua masuala yanayohusu AZAKI kuanzia kusajiliwa, namna ya kufuata Sheria na Sheria zenyewe, kwa hiyo itawasaidia sana wadau kuweza kufahamu maeneo tofauti ya kufanya kazi kwa kufuata Sheria” amefafanua.

Ameongeza FCS inajipanga kuandaa mkutano mkubwa zaidi kwa kushirikisha wadau wengi ili kuendelea kutoa uelewa juu ya sheria hizo kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Serikali kama TRA, NSSF, OSHA, WIZARA YA KAZI na Taasisi nyingine za Serikali ili kuendelea kukuza uelewa mpana zaidi.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa Asasi za Kiraia zilizoshiriki mkutano huo zimesema kuwa zimepokea maboresho ya Sheria hizo na kwamba wanahakikisha wanafuata sheria inavyosema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...