Baada ya Mapumziko ya takriban wiki tatu Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea tena leo kwa michezo miwili kupigwa katika Viwanja viwili tofauti.

Katika mchezo wa kwanza utakaopigwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya itazikutanisha timu ya Mbeya City akikmaribisha Kagera Sugar mechi itakayopigwa kuanzia saa 8 mchana. 

Mchezo wa Pili utawakutanisha wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa kombe la Shirikisho Namungo akiwa nyumbani kumkaribisha Ihefu kwenye dimba la Majaliwa Mkoani Lindi.

Ratiba hiyo inaonesha pia, kesho Aprili 09, inaonesha Timu ya Biashara United itamkaribisha Polisi Tanzania katika Uwanja wa Karume Mkoani Mara huku JKT Tanzania akiwa nyumbani dhidi ya Mwadui FC.

Katika mchezo mwingine Azam Fc wataikaribisha Mtibwa Mechi itakayochezwa kuanzia majira ya saa 1 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ligi Kuu itaendelea tena Jumamosu kwa michezo mitatu kupigwa katika Viwanja vitatu tofauti, Vinara wa Ligi Kuu Yanga wakiwakaribisha KMC katika Dimba la Benjamin Mkapa huku Tanzania Prisons akimkaribisha Dodoma Jijini Uwanja wa Nelson Mandela.

Mchezo wa mwingine ni Gwambina wakiwa nyumbani dhidi ya Coastal Union huku mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Simba ukisogezwa mbele kutoka na wawakilishi hao kuwa katika majukumu ya Klabu Bingwa Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...