Golikipa wa Simba SC, Aishi Manula amesema yupo tayari kwa maamuzi ya timu yake ya Simba SC kuamua yeye kubaki au kuuzwa klabuni hapo.

Manula amehusishwa kusajiliwa na Klabu ya El Merreikh ya Sudan πŸ‡ΈπŸ‡© na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini πŸ‡ΏπŸ‡¦ licha kuwa na mkataba na Wekundu wa Msimbazi.

Kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha Azam TV baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Aishi amesema yupo tayari kwa changamoto ndani au nje ya nchi kwa msimu huu au msimu ujao wa mashindano.

“Inafahamika Mchezaji akiwa na mkataba na timu fulani, kama kuna Klabu inataka kumsajili basi inafika kwa timu ambayo Mchezaji huyo ana mkataba nayo ana ana itumikia kwa wakati huo”, amesema Manula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...