Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Fatma M. Rajab leo amewasili katika Ofisi za Makao Makuu ya
Wizara zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma na kupolewa
na Watumishi na Menejimenti ya Wizara.
Balozi
Fatma Rajab baada ya mapokezi hayo alipata wasaha wa kuongea na Wakuu
wa Idara na Vitengo ambapo licha yakuwataka kuendelea kufanya kazi kwa
weledi na juhudi amewaahidi ushirikiano katika kuteleza majumu yao ya
kila siku.
Balozi
Fatma aliapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki tarehe 6 Aprili, 2021.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akipokelewa Wizarani Mtumba, jijini
Dodoma. |
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisalimiana na Balozi Anisa Mbega
alipowasili Wizarani. |
| Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisalimiana na Balozi Stephen P. Mbundi wakati anapokelewa Wizarani. |
| Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akisaini kitabu cha wageni alipowasili
Wizarani |
| Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab akiongea na Watumishi na Menejimenti ya Wizara (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili Wizarani |


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...