Charles James, Michuzi TV
MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesema ana imani kubwa kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia watanzania kwani ameonesha uwezo wa uongozi toka alivyoapishwa kuwa Rais na hata alivyokua Makamu wa Rais.
Kingu ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokua akitoa maoni yake ya uongozi wa Mama Samia ambapo amewataka watanzania kumuamini kwani ana uwezo mkubwa wa uongozi.
Amesema toka kuingia kwa Mama Samia tayari yeye kwenye Jimbo lake ameshaletewa kiasi cha Sh Bilioni Tatu kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo jambo linaloonesha jinsi gani amepanga kuwatumikia watanzania kwa nguvu na kasi zaidi.
" Sina shaka na uwezo wa Mama amekuepo Serikali kwa muda mrefu na tunapoona mafanikio tuliyonayo kwa miaka mitano hii basi Mama amechangia kwa kiasi kikubwa kwani nae alikua sehemu ya uongozi, niwatoe hofu watanzania kwamba tuna Rais hodari na mwenye uwezo," Amesema Samia Suluhu.
Akizungumzia suala la baadhi ya wanasiasa kubadilisha msimamo wao wa Corona, Kingu amesema ni kweli ugonjwa huo upo lakini ni ukweli usio na shaka kwamba njia ya kujifukiza imesaidia sana watanzania wengi.
" Hatuwezi kukataa kwamba Corona ipo lakini njia ya kujifukiza ilitusaidia wengi, nitoe rai kwa sisi vijana kuwa na misimamo na kauli zetu ambazo tunakua tunazitoa ili kuendelea kuaminika kwa wananchi, " Amesema Kingu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...