Na WAMJW- Dom

Mganga Mkuu wa Serikali ametakiwa kusimamia mifumo ya uwajibikaji katika sekta ya afya nchini ili kupunguza vifo vya wajawazito pamoja na kupanua huduma za kibingwa ikiwemo vifaa vya kisasa ili kuvutia nchi za jirani kupata huduma za afya hapa nchini

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Afya), Prof. Abel Makubi, leo tarehe 9 Aprili,2021 wakati  akimkabidhi ofisi Mganga Mkuu wa Serikali  Dkt. Aifelo  Sichalwe kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali  iliyopo katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Prof. Makubi ambaye alihudhumu nafasi ya Mganga Mkuu wa Serikali  hapo awali amempongezà Dkt. Sichalwe kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.

Aidha, Prof. Makubi amemtaka CMO huyo kusimamia  kusimamia suala la dawa, vifaa na vifaa tiba, kupambana na magonjwa yasiyoambukiza,  huduma za tiba asili,  ujenzi wa miundombinu pamoja na kusimamia mwenendo wa kuanza kwa Bima ya Afya kwa wote.





 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...