MSANII  Nyota Akachukwu Emmanuel  Uche maarufu MMZY anayekuja kwa kasi chini ya Lebo ya Kerae Records Akachukwu.

Uche 'MMZY' ameachia rasmi EP yake ya kwanza iliyopewa jina la ASCENT EP yenye nyimbo 8

Ni msanii ambaye anakuja vizuri kupitia Muziki aina ya Afrobeat akiwakilisha nchini Nigeria, licha ya msanii huyo kuwa na ubora katika uandishi wake, sauti yake ni moja ya kitu kinachomtofautisha na wasanii wengine ambao wamewahi kutokea katika muziki nchini Nigeria.

MMZY ameachia rasmi EP yake ya kwanza iliyopewa jina la ASCENT EP yenye nyimbo 8 huku ikiwa mbili ameshirikisha  kwa kushirikiana na msanii wa muziki Teni pamoja na Terri.

ASCENT EP imetayarishwa na watayarishaji watano ambaye ni Masterkraft,Echo The Guru,Cranker Mallo,Blaise Beats,Ozedikuz na nyimbo zote kukamilishwa na mtayarishaji Mix Monster.

Nyimbo zote zimeandikwa na msanii MMZY isipokuwa aliyoshirikiana na Teni pamoja na Terri na bila kusahau wimbo namba 3,4,5,8.

Kati ya nyimbo hizo wimbo wa Dominate ni  wimbo wake unaofanya vizuri kwa sasa ukiwa unapatikana pia ndani ya EP yake hiyo iliyopewa jina la ASCENT.

Kuwa wa kwanza kusikiliza kazi zote kutoka kwenye EP kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo,apple music,boomplay,spotify,audiomack na youtube.

MMZY unaweza kumpata kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram @therealmmzy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...