Na Jumbe Ismailly SINGIDA .

MWANAFUNZI wa darasa la sita katika shule ya msingi Minga,Manispaa ya Singida,Paschali Stephano Emaanueli amenusurika kufa baada ya askari mmoja kumwagia mafuta aina ya petroli na kisha kumchoma moto kwa madai ya kumtuhumu kuwa ameiba dumu la lita tano la mafuta aina ya alzeti na kujaribu kuliuza kwa abiria wanaokwenda vijijini.

Paschali mwenye umri wa miaka 14 ni mtoto wa mama mwenye ulemavu wa mikono yote miwili,Jackleen Hasani alipatwa na mkasa huo Apr,02,mwaka huu saa saba mchana kwenye kituo kidogo cha mabasi,yaendayo vijijini,maarufu kwa jina la stendi ya vumbi muda mfupi baada ya kuwasili akitokea uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Mwenge alipokuwa akifanya mazoezi ya mchezo wa mpira wa miguu.

Alifafanua mwanafunzi huyo kwamba siku ya tukio wakati akielekea kwenye soko la kimataifa la vitunguu alikutana na mtu mmoja asiyemfahamu jina lake na kumuomba amsaidie kubeba galoni nne za mafuta ya alzeti na kumuahidi kumpatia ujira wa shilingi 1,000/= kwa kila geleni.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo aliridhia kubeba geleni kutoka kwenye soko la kimataifa ya vitunguu hadi kwenye stendi ya vumbi na kutakiwa kulirudisha tena geleni hilo alikokuwa amelitoa kwa madai kwamba alikwisha agiza mafuta mengine.

Hata hivyo Paschali alisisitiza kuwa alipolirudisha ndipo alipokutana na mwenye mafuta ambaye alimpelekea mteja wake na ndipo ghafla askari alitokea na kukaa pembeni na mwenye mafuta hayo na kisha kufanya mazungumzo na kushuhudia askari huyo akipokea shilingi 70,000/= ambazo hata hivyo hakujua walikuwa wamefanya biashara gani.

Alisisitiza kwamba baada ya askari huyo kupokea kiasi hicho cha fedha ndipo mwenye mafuta aliondoka na kubaki yeye na askari huyo na ndipo ghafla alichukua Petroli kwenye pikipiki na kumwagia mwanafunzi huyo na kuwasha kiberiti naye kuanza kuungua na kuzitaja sehemu alizoathirika kuwa ni pamoja na sehemu za siri,kwenye kisigino cha mguu na mguu mmoja kwa nyuma.

Hata hivyo Paschali aliweka wazi kwamba baada ya kuanza kuungua moto huo ndipo alitokea msamaria mwema aliyemtaja kwa jina moja tu la Fadhili na kumpiga teke ambalo lilimwezesha kuangukia kwenye maji na moto huo ukazimika,na ndipo baada ya hapo alikwenda kuripoti kituo kidogo cha polisi kilichopo kituo cha mabasi yaendayo mikoani na ndipo askari wa kituo hicho walimwamuru aliyemtuma mafuta agharamie matibabu badala ya askari aliyemchoma.

“Kidonda cha kwenye kisigino ndicho bado kinanisumbua na nashindwa hata kutembea vizuri,hivyo naiomba serikali isilifumbie macho suala hilo kwani mimi nashangaa askari mwenye kujua sheria ndiye anayezivunja kwa kujichukulia sheria mkononi”alisisitiza Paschali.

Mama mzazi wa Paschal,Jackleen Stephano Hassani (38) mkazi wa Mtaa wa Mnung’una,Manispaa ya Singida ni mama mwenye ulemavu wa mikono alisema siku ya tukio ilikuwa siku ya ijumaa kuu naye alikuwa kanisani na kuwakuta watu wamejaa nyumbani kwake na hivyo alitaka kufahamu sababu za kuwepo kwa watu hao nyumbani kwake.

Alibainisha Jackleen ambaye ni muimbaji wa kwaya ya Usharika wa Nazareti Mitunduruni kwamba ndipo alielezwa kwamba kuna tukio la mtoto wake kuchomwa moto na askari na alipomwangalia mwanaye,roho yake iliumia sana na ndipo alipoingia ndani na kuanza kuomba.

“Kwa kweli nilipomwangalia mtoto roho yangu iliumia sana nikaingia ndani nikaanza kuomba,nilipoomba na siku iliyofuata nilipoamka nikaenda nikawashirikisha kwaya ya Amkeni,Usharika wa Nazareti ambao bado tunaendelea mpaka sasa kumwombea kijana wangu”alisisitiza huku akionesha masikitiko.

Jitihada za kumpata askari Albert Ngoda ili azungumzie tuhuma hizo hazikuzaa matunda baada ya simu yake yenye namba 0769-020 477 kutopatikana licha ya kupigwa kwa zaidi ya safari tano.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida,ASP Sweetbert Njewike alipotakiwa kuzungumzia tuhuma za askari huyo aliahidi kufuatilia taarifa hiyo licha ya kuwa nje ya Mkoa kikazi lakini atamwagiza kaimu kamanda aliyemwachia ofisi ili aweze kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...