Jane Edward, Michuzi TV, Arusha
SERIKALI imekitaka Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS )kuacha kujihusisha na masuala ya kisiasa na uanaharakati badala yake kijikite zaidi kusaidia jamii katika nyanja za kisheria.
Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Sheria na Katiba,Amon Mpanju,aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa TLS unaoendelea jijini Arusha,ambapo pamoja na Mambo mengine Mkutano huo utamchangua rais mpya kuchukua nafasi ya aliyemaliza muda wake.
Mpanju ambaye kitaaluma ni wakili,alisema kuwa kumekuwepo na Baadhi ya Viongozi wanaochaguliwa na TLS kuendesha harakati za kisiasa na kusahau majukumu yao Jambo hilo lisifanyike na chama hicho kijikite kutetea haki za wananchi.
Amewataka wanachama wa TLS wanaofikia 10,000 hapa nchini kuzingatia maadili ya taaluma yao ,kuwa na mienendo mizuri Katika kufuata utawala wa kisheria.
"Kuna mawakili wamekuwa na tabia ya kuchukua fedha za wateja wao na kushindwa kuwawakilisha vizuri na wengine kutelekeza mashauri yao,Jambo Hilo si jema Sana na wanapaswa kubadilika na kuzingatia miiko ya kazi yao"alisema.
Katika hatua nyingine Mpanju ameonya mawakili wa serikali wapatao 1703 ambao Baadhi yao wanajihusisha na uwakili wa kujitegemea nje na utaratibu, kuacha Mara moja na kuwataka wenye tabia hiyo kuchagua moja Kati ya uwakili wa serikali ama kujitegemea.
Ameitaka TLS kujikita zaidi kwenye misingi ya kuendeleza tasinia ya kisheria na Viongozi wanaochaguliwa wajitafakari na kuja na mbinu mpya ya kuwatetea wananchi.
Awali Rais wa TLS anayemaliza muda wake, Dkt Rugemereza Nshalla,amesema kuwa TLS imekuwa na Changamoto mbalimbali hali iliyofanya kushindwa kufikia malengo yake Katika kipindi cha miaka
miwili.
Alizitaja Baadhi ya Changamoto hizo kuwa ni pamoja na mabadiliko ya kisheria hapa nchini,Ugonjwa wa Corona ,Baadhi ya wanachama kubambikiwa kesi zikiwemo za utakatishaji fedha,wanachama kutishwa na wengine kufutiwa leseni ,kuhuisha leseni na kutakiwa kujisajili Kodi
ya ongezeko la thamani (VAT).
Hata hivyo dkt Nshalla alisisitiza kuwa TLS itaendelea kupigania na kutetea haki za wananchi pamoja na wanachama wake ikiwemo wanachama waliofungiwa leseni zao.
Chama hicho Cha wanasheria Tanganyika kinatarajia kufanya uchaguzi hapo kesho(leo) kumpata rais mpya baada ya Dkt Nshalla kumaliza muda wake,ambapo wagombea watano watachuana vikali kuwania nafasi hiyo ambao ni Albert Msando,Dkt Edward Hosea,Flaviana Charles,Fransis Stolla na Shehzad Walli.
Naibu katibu Mkuu wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju, akizungumza na waandishi wa Habari, Mara baada ya kufungua Mkutano wa Chama cha mawakili wa kujitegemea Tanganyika (TLS)Picha na Jane Edward, Michuzi TV, Arusha)
Picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...