Na Mwandishi wetu, Manyara
NAIBU
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, mhandisi Godfrey Kasekenya, ameipongeza
Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoani Manyara kwa namna
wanavyotunza, kukarabati na kutengeneza barabara za eneo hilo.
Akizungumza
baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Manyara, Mhandisi
Kasekenya amempongeza Meneja wa TANROADS Mkoani Manyara mhandisi Bashiri
Rwesingisa.
Amesema
anakiri kukutana na wabunge wa mkoa wa Manyara na wameridhishwa na namna
TANROADS Manyara wanavyozihudumia barabara zilizopo chini yao na yeye
binafsi amejionea hali halisi.
“Wabunge
ni wanasiasa na wanaposifia jambo ni kweli kuna kazi imefanyika hivyo
nawapongeza TANROADS Manyara kwa namna mnavyofanya kazi hadi wabunge wa
mkoa wenu wanawapongeza,” amesema mhandisi Kasekenya.
Amesema
katika ziara yake ya siku mbili ametembelea daraja la Magara
linalounganisha Wilaya za Babati na Mbulu, barabara ya Mbulu-Haydom,
barabara ya Haydom-Mogitu Wilayani Hanang’ na barabara ya Singe
Babati-Kimotorok wilayani Simanjiro inayofika hadi wilayani Kiteto.
“TANROADS
Manyara nawapongeza mno, kwa namna mnavyotekeleza wajibu wenu katika
kuhudumia barabara zote za mkoa mnazozisimamia, hongereni sana,” amesema
mhandisi Kasekenya.
Hata
hivyo, Meneja wa TANROADS Mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa
akitoa taarifa kwa Naibu Waziri huyo amesema wanakabiliwa na changamoto
ya uhaba wa kokoto kwa makandarasi wanaotengeneza barabara.
Mhandisi
Rwesingisa amesema kutokana na uhaba wa kokoto hizo inawalazimu
makandarasi kuzisafirisha kutoka Mkoani Mwanza au Wilayani Bukoba mkoani
Kagera.
Ametaja
changamoto nyingine ni ukosefu wa wakandarasi wenye uwezo wa kazi za
madaraja, hali inayosababisha baadhi ya makandarasi kuikimbia miradi.
Meneja wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS) Mkoani
Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa akisoma taaarifa kwa Naibu Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi mhandisi Godfrey Kasekenya.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi mhandisi Godfrey
Kasekenya (kushoto) akikagua barabara ya Singe-Kimotorok baada ya
kumaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Manyara, ambapo ametembelea
Wilaya za Babati, Mbulu na Hanang’, kulia ni Meneja wa Wakala wa
barabara nchini (TANROADS) Mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...