Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul jana April 24,/2021 amefanya  ziara katika Tasisi  za Wizara hiyo za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Gekul ametoa maelekezo yafuatayo:

1) Baraza la Sanaa la Taifa - BASATA kukamilisha mfumo wa kielektroniki wa usajili wa wasanii wote nchini, Baraza kusimamia maadili ya wasanii ipasavyo, Baraza kufufua muziki  wa asili wa watanzania pamoja na Baraza kuwa rafiki kwa wasanii na kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara,

2) Aidha Mhe. Gekul alipoitembelea Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ambako alipokea changamoto mbali mbali zinazoikabili kampuni hiyo huku akisisitiza TSN kuchapa kazi kwa bidii na kuendelea na kazi ya kuwahabarisha Watanzania juu ya miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita kwa ujumla.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...