Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amepokea  viatu 120 kwa ajili ya wanariadha kutoka  Shirika la Kimataifa la Maendeleo la nchini Japan (JICA) katika hafla iliyofanyika leo tarehe 16/04/2021 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kupokea vifaa hivyo mbele ya viongozi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Mhe. Gekul amesema " Tunawashukuru JICA kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika sekta ya Michezo hususani mchezo wa riadha, JICA wamekuwa wadau wakubwa katika kuendeleza mchezo wa riadha hapa nchini ambapo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa wamedhamini mashindano ya riadha kwa wanawake ya "Lady's First" pamoja na kutoa utaalamu".

"Serikali inatambua suala la michezo ni ajira, kazi na afya hivyo tutasimamia na kutatua changamoto wanazozipata vyama vya michezo ili kuendeleza michezo kwa taifa letu," amesema Pauline.

Aidha Mhe.Pauline ameitaka RT kuhakikisha viatu hivyo vinatolewa kwa watu sahihi pamoja na kushirikiana vyema na Taasisi ya JICA kuandaa mashindano mbalimbali nje ya Dar es Salaam ili kuibua vipaji vipya vya wanariadha hususani kwenye mikoa yenye vipaji vya riadha.

"Nina imani mikoani kuna wachezaji wazuri lakini hawafikiwi hivyo naomba RT  kwenda huko kutafuta vipaji kwa ajili ya kuandaa timu bora ya Taifa"

Mhe. Pauline amesema Serikali itashirikiana bega kwa bega na RT kuhakikisha maandalizi ya Timu ya Taifa ya Riadha iliyopo kambini jijini Arusha kujiandaa na Mashindano ya Olympic nchini Japan yanakwenda vizuri.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Pauline amefungua mafunzo kwa viongozi wa vyama vya michezo kwa wenye ulemavu na amewataka viongozi hao kutumia vizuri mafunzo wanayopata kuhusu utawala bora ili kuendesha vyama vyao kwa weledi na kuwa wazi katika matumizi ya fedha.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...