Na Mwandishi wetu, Hanang'
MRATIBU
chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara, Mkojera
Philemon Mkojera amenusurika kwenda jela miezi 12 baada ya Mahakama ya
Hakimu mkazi wa Wilaya hiyo, kumhukumu kulipa faini ya sh950,000 kwa
kosa la kughushi.
Hakimu
Mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Hanang' Samwel Mushumbusi ametoa hukumu
hiyo kwenye mahakama hiyo ya kulipa faini hiyo ya shilingi 950,000 kwa
makosa 19 ya rushwa na kufanikiwa kuepuka kifungo cha miezi 12.
Hakimu
Mushumbusi ametoa hukumu hiyo kwa makosa ya kughushi kinyume na kifungu
cha 333,3335 (a) 337, vya sheria ya kanuni ya adhabu na ubadhirifu
kinyume na kifungu cha 28 (1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na
rushwa namba 11/2007.
Mratibu
huyo wa chanjo wa halmashauri ya wilaya ya Hanang' Mkojera, amelipa
faini ya shilingi 50,000 kwa kila kosa kati ya makosa 19 aliyoshtakiwa
kwa kughushi.
Hata hivyo,
Mkojera anatarajiwa kufikishwa tena mahakamani kwa makosa mengine ya
matumizi ya nyaraka ya kumdanganya mwajiri wake kinyume na kifungu cha
22, ubadhirifu kinyume na kifungu cha 28 (1) cha sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 1/2007 pamoja na uhujumu uchumi tofauti na
kesi aliyohukumiwa Machi 31.
Awali,
Mkojera alifikishwa mahakamani hapo na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Martin Makani na Eveline Onditi kwa
makosa 19 yakiwemo ya kughushi na ubadhirifu wa fedha.
Mkojera
alifanya makosa hayo Octoba 2014 katika maeneo mbalimbali Wilayani
Hanang' kwa kughushi majina na sahihi za watu 18 kuwa aliwalipa posho
watu 10 shilingi 240,000 kila mmoja na watu nane shilingi elfu 70
wakati wa chanjo ya surua na rubela.
Hata
hivyo, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu ameelekeza
endapo Mkojera hajaondolewa katika utumishi wa umma basi halmashauri ya
Hanang' ianze mchakato wa kukuondoa kwenye utumishi wa umma kwa mujibu
wa kanuni ya utumishi wa umma za mwaka 2003.
Makungu
amesema Mamlaka hiyo ya nidhani iangalie kwamba kwa mujibu wa kanuni za
kudumu za utumishi wa umma za 2009 kanuni F39 (3) mtumishi wa umma
akipatikana na hatia ya makosa ya jinai yatokanayo na rushwa na
ubadhirifu wa fedha au mali ya umma, kama ilivyo kwa Mkojera hupoteza
stahili zake zote katika utumishi wa umma.
"Ni
rai yetu kwa watumishi wa umma kujiepusha na vitendo vya rushwa na
ubadhirifu ili kuepuka kupoteza haki zao kwenye utumishi wa umma kama
Mkojera atakavyopoteza kutokana na ubadhirifu wa shilingi 2660,000
alioufanya," amesema Makungu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...