ILI kuhakikisha Sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji wanafikia uwezo mkubwa wa kupata zana bora na za kisasa za kilimo kampuni ya Pass Leasing kupitia kampuni tanzu ya Private Agricultural Sector Support ( PASS) imeanzisha mpango wa kumilikisha zana hizo kwa mtumiaji kupitia njia ya kukodisha ama kukopesha kwa bei nafuu na masharti rafiki.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (PASS) Anna Shanalingigwa ameyasema hayo leo Aprili 15, 2021 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za PASS Trust zilizopo jijijini Ilala Mkoani Dar es Salaam juu ya Kampuni mpya ya Pass leasing yenye lengo la kuwanufaisha wakulima, wavuvi na wafugaji kwa kuwawezesha kupata mikopo bila dhamana na kwa gharama za chini.

Amesema, lengo kuu la PASS Trust ni kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na maendeleo ya kibiashara kwa wajasiriamali wa biashara za kilimo, mifugo na uvuvi katika mnyororo mzima wa thamani.

Akielezea namna wanufaika watakavyofaidika Anna amesema, PASS Trust itatoa dhamana ya mikopo kuanzia asilimia 20 hadi 60 na hadi 80 kwa wanawake kwa benki shirika kama njia ya kuongeza dhamana ya kutosha ili kuwawezesha wateja kupata mkopo na kufikia lengo lao la kuwafikia watanzania wengi huo utakavyokuwa.

"Tangu kuanzishwa kwa PASS Trust mwaka 2000 wameishadhamini miradi 46,300 yenye thamani ya takribani trilioni moja ambapo jumla ya wajasiliamali milioni 1.7 wamenufaika na miradi hii huku pia tukijivunia kutengeneza fursa za ajira milioni mbili ambazo zimeboresha maisha ya watanzania." Amesema Anna.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PASS Leasing, Killo Lusewa amesema, kampuni hiyo imepata kibali rasmi cha uanzishaji shughuli za mikopo ya zana za kilimo na vifaa vinavyoshabihiana kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kwamba usajili huo utaiwezesha kampuni hiyo kuweza kufanya kazi zake ndani ya Tanzania.

Amesema, PASS itatumia mpango wa kukodisha ama kukopesha wateja vifaa kwa bei nafuu ili kuhakikisha wazalishaji wa sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji wanafikia uwezo wa kupata zana bora na za kisasa ambazo mwisho wa siku watazimiliki wao wenyewe.


Amesema Mkopaji atatakiwa kutanguliza asilimia 20 ya zana anayokopa na asilimia 80 itakayobaki atailipa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi mitatu kutokana na kifaa atakachokua.

Amesema walengwa wakubwa wa mradi huo ni wakulima na wajasiliamali wanaojishughulisha na kilimo kwaujumla ikiwemo kilimo cha mazao, umwagiliaji, uvuvi, ufugaji wa wanyama na nyuki, misitu usafirishaji uhifadhi pamoja na usindikaji wa vyakula.

"Kupitia kampuni yetu wateja watanufaika na huduma bora kwa kuhudumiwa na wataalamu waliobobea kwenye sekta ya mikopo na kilimo, na pia watapata huduma kwa wa wakati huku pia wakimiliki vifaa kwa gharama nafuu bila kuweka dhamana yoyote." Amesema Lusewa.

Amesema, lengo kubwa la kampuni hiyo kwa mwaka huu ni kuhakikisha wakopaji 300 wanafikiwa na kupatiwa zana za kilimo na zile zinazoshabihiyana nazo ambapo wanatarijia kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 12 na kuwanufaisha zaidi ya wakulima na wazalishaji elfu 12 na kutengeneza nafasi za ajira kwa watu wasiopungua 600.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Private Agricultural Sector Support (Pass), Anna Shanalingiwa akimkabidhi kibali rasmi cha uanzishaji wa shughuli za mikopo ya zana za Kilimo kwa kampuni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PASS Leasing, Killo Lusewa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Aprili 15,2021 katika ofisi za PASS zilizopo jijini Ilala mkoani Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Private Agricultural Sector Support (Pass) Anna Shanalingiwa akizungumza wakati wa kuitambulisha kampuni mpya ya PASS Leasing yenye lengo la kuwanufaisha wakulima, wavuvi na wafugaji kupata mikopo bila dhmana.
Mtaalamu wa mawasiliano wa kampuni za PASS Trust na PASS Leasing,  Bevin Bhoke (aliyesimama) akizungumza  wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya kuanzishwa kwa kampuni mpya ya PASS Leasing kwa ajili ya shughuli za mikopo ya zana za kilimo uliofanyika leo Aprili 15, jijini Ilala mkoani Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...