Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

JESHI  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam katika kipindi cha kuanzia Mwezi Machi hadi Aprili 2021 limefanya oparesheni ya kupambana na wahalifu vinara wanaojihusisha na wizi wa magari na pikipiki katika jiji la Dar es salaam.

Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kufanyika oparesheni hiyo iliyofanyika katika maeneo mbalimbali jijini.

Amesema kuwa  Jeshi la Polisi Kanda Maalum limefanikiwa kukamata watuhumiwa Seleman Seif( 52)  Mkazi wa Toangoma Mbagala, Dickson Kalikila ( 47) Mkazi wa Kyela Mbeya ,Jafeth Mwaipopo( 57), Mkazi wa Kivule, Peter Philipo (32)Mkazi wa  Sinza, Omari Komba( 32) Mkazi wa Kilungule Kimara na  Abdallah Issa( 18) Mkazi wa Kibada kigamoni.

Mambosasa amesema kuna watuhumiwa wengine 7 ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.Watuhumiwa hawa walikamatwa na  magari ya wizi  ambayo ni T 387 CKD Suzuki,T 775 APA Toyota Carina,T 949 BRF Toyota Prado, T.627 DJY Toyota IST,T459 DGP Toyota Ractus,T 373 DMR Toyota Crown na T920 DRY aina ya  Nissan.

Ameongeza kwamba magari mengine 5  ambayo uchunguzi wake bado unaendelea hatutaweza kuyataja namba zake za usajili  kwa sababu za kiupelelezi.Watuhumiwa wote pamoja vielelezo wamekamatwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na Mikoa mingine.

"Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na majalada  yatapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua za kisheria. Aidha katika oparesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 41 walikamatwa wakiwa na pikipiki 28 zidhaniwazo kuwa za wizi.  

"Katika oparesheni hiyo tulifanikiwa kumkamata mwizi maarufu wa pikipiki anayefahamika kwa ajina la Hamisi Beatus marufu Masai (27) mkazi wa Manzese  Dar es Salaam na Ifakara mkoani Morogoro ambaye ndiye kinara wa wizi pikipiki katika mikoa ya Dar es salaam     na Morogoro,"amesema.

Ameongeza  mtuhumiwa huyu alihojiwa na kukiri kuhusika kushiriki kuiba na kupokea pikipiki mbalimbali za wizi kutoka kwa washirika wake waliopo jijini Dsm na Mkoa wa Morogoro. Mambosasa ametoa mwito kwa jamii, wananchi wanatakiwa kuwa makini na magari yao hasa maeneo ya kuegesha ambayo hayana uangalizi au ulinzi wa kutosha.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...