Na Jusline Marco-Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddy Kimanta amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi kutenga siku maalum ya vyuo vyilivyomo ndani ya jiji la  Arusha kufanya mazoezi ya pamoja ili kuboresha afya sambamba na kujenga Mkoa huo.

Akiongoza mbio hizo za kilometa 6, Mkuu huyo wa Mkoa ameupongeza uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kuadhimisha siku ya Muungano kwa kufanya mazoezi ya mbio fupi ambapo amevitaka vyuo vingine vilivyopo mkoani humo kuiga mfano huo kwani mazoezi ni afya hivyo amekiomba chuo hicho kuyafanya mbio hizo kuwa mwendelezo.

Aidha  mbio fupi maarufu kama mbio za (Fun run) kuelekea Marathon ya kitaifa inayotarajiwa  kufanywa na  chuo hicho mwezi Juni mwaka huu ambapo alisema ushirikiano mzuri utapelekea kuijenga Arusha kulingana na maagizo ya Mhe,Rais Samia Suluhu aliyoyatoa wakati akiwa makamu wa Rais na kusema huu niwakati wa kuimarisha vikundi vya mazoezi ili kuweza kukabiliana na changamoto ya COVID 19 kwani ni sehemu ya dawa.

“Pamoja na kutafuta siku maalum kwaajili ya vyou kufanya mazoezi lakini pia vyuo vingine viige mfano wa IAA kwani pamoja na kutoa elimu lakini pia wanaboresha afya za wanafunzi wao, watumishi na watu wengine majirani wakiwemo wakuu wa tasisi kwa kufanya mbio hizi,” Alisema Kimanta.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi alikitaka chuo hicho kuendelea kufanya mambo ambayo yataweka wanaarusha pamoja na kujenga afya zao itakayo wasaidia kuepuka magonjwa nyemelezi na kuwataka wengine kuiga suala hilo ili kuboresha afya za wanajamii.

Naye mkuu wa chuo hicho Prof.Eliamani Sedoyeka alisema kuwa mbio hizo ni mwendelezo wa fun run wanazozifanya kila mwezi kwaajili ya maandalizi ya mbio kubwa zitakazofanyika mwezi juni meska huu kwa kushirikisha watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Aliongeza kuwa IAA marathon imelenga kutangaza chuo kwani ndio msingi mkubwa wa biashara ambapo wanapokuwa wamekikuza chuo watakuwa na mvuto zaidi kwa wateja na hiyo ni moja kati ya mikakati yao kwa kuja na shughuli za kitaifa ambazo zitaweza kuvutia watu wengi zaifi.

Alisema kupitia mbio hizo wataweza kunyanyua na kukuza vipaji vya kukimbia kwani nchi ya Tanzania kwa kipindi cha hivi karibuni imekuwa kama kivutio cha watu kufahamiana, kuwa na undugu lakini pia kushereheka zaidi ambapo Arusha iko nyanja za juu kuyokana na  maeneo yake kuwa mazuri kwa  kufanya mazoezi ya mbio ndefu hivyo wanategemea yataleta upizani mkubwa.

Aidha alisema kuwa mazoezi hayo ni muhimu kwa mwanagunzi au mwalimu kuweza kuwa na akili nzuri katika kufundishwa au kujifunza na kuweza kuondoa mawazo ambapo alisema wamejipanga kuhakikisha kuwa wale wote watakao waalika watawashindanisha na kutoa mabingwa ambao wataweka rekodi za kitaifa kwenye kilometa 21 na 47.

"Pamoja na kuondoa stress lakini pia mazoezi hujenga mwili kwa kuweka vizuri  usawa wa sukari, chumvi  na madini  mengine yaliyo mwilini pamoja na kuchochea unywaji wa maji  ambao unapelekea kuweka misuli na damu sawa pamoja na kuondoa yale magonjwa yasiyoya kuambukizia kama sukari, moyo, msogo wa mawazo na mengine," Alisema Prof.Sedoyeka

Kwa upande mwingine makamu wa raisi wa chama cha riadha nchini John Bayoa ambaye alikuwa ni mmoja wa washiriki katika mbio hizo alisema kuwa mbio hizo zitakuja kuwa kubwa ikiwa ni pamoja na kuwataka kuwashirikisha wataalamu katika maandalizi ili kuepuka kushindwa kukidhi vigezo ambavyo vitawapelekea kufungiwa .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddy Kimanta wa pili kulia akiongoza akiongoza wakazi wa jiji la Arusha katika mazoezi yaliyoandaliwa na uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha.

Wakazi wa jiji la Arusha na wanachuo wa chuo cha uhasibu Arusha wakifanya moja ya mazoezi katika mbio fupi hizo.
Viongozi wa Mkoa,wilaya na chuo cha IAA kwa pamoja wakiwa katika mbio fupi zilizofanyika jijini Arusha.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...