Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo ameshiriki Mashindano ya Sita ya Kuhifadhi Quran takatifu ambapo ametoa wito kwa Mashirika yaliyopewa usajili kwa lengo la kusaidia jamii hususani yatima na wasiojiweza kuhakikisha wanatenda haki kwa walengwa.

RC Kunenge amesema haipendezi kuona Shirika linapokea msaada wa vitu kwaajili ya kuasaidia Yatima, Makundi maalumu na waishio Katika Mazingira Magumu na kutumia msaada huo kujinufaisha wenyewe pasipo kuwafikia walengwa ambapo amesema kitendo hicho ni "ubabaishaji".

Aidha RC Kunenge amesema ndani ya Jamii tumebarikiwa kuwa na Wadau wengi wanaopenda kusaidia watu wasiojiweza lakini uwepo wa Taasisi zisizofuata misingi ya usajili imekuwa ikiwavunja moyo Wadau.

Akizungumza kuhusu Mashindano hayo RC Kunenge amesema yanasaidia Jamii kuelewa kwa undani Vitabu vya dini Jambo linalojenga Jamii yenye maadili na hofu ya Mungu.

Hata hivyo RC Kunenge ameipongeza Taasisi ya Faraja Islamic Foundation kwa chini ya Mkurugenzi wake Hashim Madenge kwa kuona umuhimu wa kuandaa Mashindano ya Kuhifadhi Quran takatifu ambapo amesema Serikali itampatia ushirikiano sababu anachokifanya kina manufaa kwa wananc
hi.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...