Na.Khadija Seif, Michuzi
WANDAAJI Wa Shindano la urembo (Miss Kilimanjaro) Wameeleza Siri ya kutoa warembo Wenye nidhamu.
Akizungumza na Michuzi Tv Dotto Sang'wa Mwenye dhamana ya Kuandaa Shindano hilo amesema Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe, Anna Mghwira amekua mstari wa mbele kutoa Ushirikiano wa hali ya juu kwenye Michezo hasa Sekta ya urembo.
"Mama Mghwira amekua akijitolea Sana hadi anapata walau muda wa kutembelea kambi ya warembo wetu na kutumia muda wake kuwafundisha vingi ikiwemo maadili na nidhamu, ili wanapotoka hapa na kuelekea Miss Tanzania waendelee kujijengea sifa njema ."
Hata hivyo Sang'wa amesema kwa Mwaka huu wanatarajia Kuanza Mchakato wa kumtafuta Miss Kilimanjaro mwanzoni mwa Mwezi Mei.
"Kutokana na Mkurugenzi wa The Look Basiila Mwanukuzi amezindua rasmi Mashindano hayo na kutupa semina elekezi ni fursa nyingine kuendelea kushiriki nae katika kila Mchakato bega kwa bega ."
Pia amesema Wapenzi na wadau wa Sekta ya urembo wategemee taji kubakia Tena Kanda ya kaskazini Kama alivyoweza Kunyakua taji Hilo Rosemary Manfere 2020.
Muandaaji wa Mashindano ya Miss Kilimanjaro Dotto Sang'wa akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam Mara baada ya Kufunguliwa kwa Mashindano ya Miss Tanzania pamoja na Semina Kwa Waandaji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...