Na Muhammed Khamis

Mwenyekiti wa kamati ya kilimo biashara na utalii kutoka Baraza la wawakilishi Ali Suleiman Ameir amesema wakati utekelezaji wa mradi wa viungo ukiendelea kuna haja watendaji kuhakikisha wanafanya kazi hio kwa moyo wa uzalendo ili uweze kuleta tija zaidi kwa wananchi na Serikali kwa ujumla.

Aliyasema hayo wakati wa kikao maalumu katika ofisi za utekelezaji huo Mwanakwerekwe mjini Unguja kufuatia kikao kilichokua la lengo la majadiliano ya kufanya ushawishi wa kisera kuhusu sekta ya kilimo.

Alisema wakati mradi huo unatekelezwa watendaji wanapaswa kutambua kuwa wana wajibu wa kuhakikisha wanapata matukio chanya ya mradi huo kinyume na miradi mengine ambayo imeshindwa kufanya vizuri.

Pamoja na hayo alisema ipo haja kuhakikisha kuwa wanufaika wa mradi huo ni walengwa husika na sio watu wengine kwa lengo la kuondoa chanagamoto mbali mbali.

‘’Lazima tutambue kuwa jamii na Serikali kwa ujumla ina matumaini makubwa na mradi huu kwa maslahi ya wananchi wake hivyo lazima mufanye kazi kwa umakini sana’’aliongezea.

Kwa upande wake mtalamu wa maswala ya kilimo Salum Rehani alisema ipo haja kwa Serikali kuweka utaratibu maalumu wa utafiti ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutambua mbegu bora za kilimo zinazopaswa kupandwa kulingana na mazingira husika.

Alisema kwa mara kadhaa Serikali imekua ikipoteza gharama kubwa ya fedha kwa kununua mbegu pamoja na mbolea lakini matukio yake faida inayopatikana haiendani na uhalisia kutoka na hasara mbali mbali wanazokutana nazo wakulima.

‘’Ninaamini kuwa iwapo utafiti utafanyika tutakua na uhakika tunalima bidhaa gani,wapi na kwa muda gani na sio watu kukurupuka tu kwa mfano unaona jinsi zao la nyanya linavoshuka bei kwa kuwa watu wote wanalima wakati mmoja’’aliongezea.

Kwa upande wake Meneja wa utekelezaji mradi huo kanda ya Unguja Bi Khadija Juma alisema Zanzibar ni sehemu iliojaliwa na fursa kubwa katika sekta ya kilimo na kwamba anaamini utekelezaji huo utaleta faida chini ya mashirikiano ya pamoja.

Aidha Meneja huyo hayo aliwaomba wajumbe wa Baraza la wawakilishi kuendelea kuishawishi Serikali kutambua umuhimu wa kuekeza zaidi katika kilimo kwani kilimo ni sekta muhimu kwa maslahi ya Taifa.

Mwenyekiti wa kamati ya kilimo biashara na utalii kutoka Baraza la wawakilishi Ali Suleiman Ameir akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.

Baadhi ya wajumebe wa mkutano wa majadiliano kuhusu sera ya kilimo wakiendelea na mkutano katika ofisi za utekelezaji wa mradi wa Viungo Mwanakwerekwe mjini Unguja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...