Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imezindua mkakati mahususi wa unywaji maziwa katika Ofisi za Umma nchini lengo likiwa ni kuongeza Soko la maziwa ya ndani lakini pia kukuza kipato cha wafugaji.

Mkakati huo umezinduliwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ambaye ametoa wito kwa watumishi wa Umma nchini na wananchi kwa ujumla kuunga juhudi mkakati huo ili pia kuimarisha ubora wa afya zao.

Waziri Mashimba amesema kwa kuanza mkakati huo utahusisha wizara 10 ambazo ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na Biashara, Tamisemi, Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Elimu.

Mashimba amesema mkakati huo wameshirikiana na Kampuni za uzalishaji maziwa ambazo zimejitokea majokofu ya kuhifadhia maziwa hayo ili yasiharibike.

" Leo tunazindua awamu ya kwanza ya unywaji maziwa kwenye ofisi za serikali na kwa kuanza tumeanza na wizara hizi 10 lakini tunaamini tutakakua na awamu zingine za uzinduzi zikihusisha wizara zingine, taasisi na mashirika ya umma.

Unywaji wa maziwa maofisini utachangia kwa kiwango kikubwa Soko la maziwa yanayotengenezwa nchini na kuepuka unywaji wa maziwa ya nje, hivyo tutakuza pato la wafugaji pia na kuchochea kiwango cha ajira kwenye Viwanda vinavyotengeneza maziwa nchini," Amesema Waziri Mashimba.

Amesema itakua ni jambo la ajabu kuona ofisi ya serikali inaagiza maziwa yanayotengenezwa nje ya nchi kwani kufanya hivyo ni kuchochea pato la nje na kukuza uchumi wa mataifa mengine.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Kazi wa nchini, Dk George Msalya amesema anaimani kama ofisi zote za serikali ambapo watumishi wa umma wanafika takribani Laki Tano zitaunga mkono unywaji huo wa mazingira itakua ni fursa nzuri na pana ya kukuza soko la maziwa ya ndani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...