Na Mwandishi Wetu
SHULE ya Msingi Hazina iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam imempongeza Rais Samia Suluhu kwa kuapishwa kuwa Rais na kupongeza kasi nzuri aliyoanza nayo.
Akzungumza, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Omari Juma amesema wadau wa elimu wana imani kubwa na Rais Samia kwamba ataendelea kusimamia na kukuza sekta ya elimu hapa nchini.
Amesema kwa uzoefu alionao, Rais Samia ataiongoa nchi kwa weledi mkubwa na kwa kushirikisha sekta binafsi anaamini sekta ya elimu itakwenda mbali zaidi.
“Sisi wadau wa elimu tunampongeza na tunaahidi kumpa ushirikiano mkubwa katika kazi zake kama rais na tunawaomba wadau wengine wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza maukumu yake,” alisema
Amesema Rais Samia amekuwa serikalini kwa muda mrefu hivyo uzoefu wake umewafanya watanzania wawe na matumaini makubwa kwamba atawavusha kwenye maendeleo ya kweli katika sekta mbalimbali.
“Shule ya Hazina imekuwa ikifanya vizuri kwenye matokeo ya Kata, Wilaya, Mkoa na Kitaiafa hivyo kwenye taaluma sisi tunaahidi kwamba tutaendelea kufundisha na kutoa elimu bora kama ambavyo tumekuwa tukifanya kama mchango wetu wa kukuza sekta ya elimu nchini,” alisema
Ametoa mfano kuwa mwishoni mwa mwaka jana wanafunzi wa shule hiyo walitia fora kwa kuongoza kwenye usaili wa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule maarufu nchini.
Amesema wanafunzi wengi wa shule hiyo waliokwenda kufanya usaili kwenye shule zenye majina makubwa walifanikiwa kuongoza na kupata nafasi za kujiunga kidato cha kwanza.
Ametoa mfano kuwa mwanafunzi aliyeongoza kwenye usaili kwenye shule maarufu ya Feza Boys alitoka Hazina na kwamba wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakiongoza kila mwaka kwenye usaili.
Amesema kwenye usaili wa mwaka jana wanafunzi sita wa Hazina walifanikiwa kufanya vizuri zaidi kwenye usaili na kujiunga na shule za Marian zilizoko Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Amesema wanafunzi sita wa Hazina walifanikiwa kufanya vizuri zaidi na kujiunga na shule za Feza wakati wanafunzi wengine tisa walifanya vizuri na kujiunga na shule ya wavulana ya Shamsiye.
“Mwaka 2019 tulipeleka wanafunzi wengi sana kwenye shule hizo na waliongoza na wazazi wengi wanapenda sana watoto wakimaliza shule ya msingi wakasome shule nzuri ndiyo sababu wanapenda kuwaleta hapa Hazina,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...