Na Mohammed Samli, Michuzi TV
BAADA ya ushindi wa bao 4-1 dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo hatimaye Klabu ya Simba imefuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) wakifikisha alama 13 wakiwa na mchezo mmoja wa mwisho wakukamilisha ratiba dhidi ya Al Ahly SC ya Misri.
Katika mchezo huo uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Benjamin Mkapa mabao ya Simba SC yalifungwa na Luis Jose Miquissone dakika ya 30, bao la pili likifungwa na Clatous Chama dakika ya 45, bao la tatu likifungwa na Rally Bwalya dakika ya 66, wakati Clatous Chama akimalizia msumari wa mwisho dakika ya 83.
Simba SC watamaliza hatua ya Makundi ya Michuano hiyo wakiongoza Kundi A, baada ya Al Ahly SC kutoa sare ya 2-2 dhidi ya wenyeji El Merreikh katika mchezo wao uliopigwa leo huko Sudan.
Hadi sasa, Simba wana alama 13, Al Ahly SC alama 8, AS Vita Club alama 4 na El Merreikh alama 2 pekee wote wakiwa na michezo mitano katika Kundi A.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...