Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Wawakilishi wa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC watacheza na Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).
Endapo Simba SC itapita hatua ya Robo Fainali itacheza na mshindi kati ya MC Algers ya Algeria au Wydad Casablanca ya Morocco kati ya Juni 18 na 19, 2021 na mchezo wa marudiano kati ya Juni 25 na 26, 2021.
Michezo mingine ni Al Ahly SC ya Misri dhidi ya Mamelodi Sundowns, MC Algers ya Algeria dhidi ya Wydad Casablanca na CR Belouzdad ya Algeria dhidi ya ES de Tunis ya Tunisia.
Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho, Pyramids FC ya Misri watacheza na Enyimba FC ya Nigeria, Orlando Pirates ya Afrika Kusini wao watapambana na Raja Casablanca Coton Sports ya Cameroon dhidi ya ASC Jaraaf ya Senegal na CS Sfaxien ya Tunisia dhidi ya JS Kabylie ya Algeria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...