Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU ),imekagua miradi 15 ya
maendeleo katika sekta ikiwemo TASAF ,maji elimu na ujenzi iliyogharimu
Bilioni 2.296.583.3 na baadhi ya miradi hiyo imebainika kuwa na dosari.
Aidha
taasisi hiyo imeokoa, fedha milioni 134.814.7 ambazo ilikuwa
zichepushwe ama kufanyiwa ubadhirifu kinyume na sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Akitoa
taarifa ya robo ya mwaka,kamanda wa TAKUKURU Pwani-Suzan Raymond
alisema wameokoa mamilioni hayo ikiwa pia ni pesa za mafao ya watumishi
na miradi ya maendeleo.
Alieleza
,kati ya miradi iliyofuatiliwa na kukutwa na kasoro ni pamoja na ujenzi
wa chuo cha VETA huko Mafia ambapo maelekezo yalitolewa kwa mamlaka
husika ili miradi iweze kuleta matokeo chanya na tija kwenye jamii.
Hata
hivyo ,kamanda huyo wa TAKUKURU anafafanua ,fedha zilizotaka
kuchepushwa ,kati ya milioni 134.814.7 ,TAKUKURU Bagamoyo iliokoa
milioni 57.722.7 michango ya mafao ya NSSF na PSSSF kwa watumishi wa
shule ya sekondari Eagle.
"Fedha hiyo ilichepushwa na haikuwasilishwa na mwajiri ambae ni mmiliki wa shule hiyo ," ofisi ilifuatiliwa na mwajiri alilipa fedha kwa wahusika ili wapate mafao yao.
Pia
alisema ,milioni 14 ziliokolewa na kutumika kuchimba visima vinne
Bagamoyo ,fedha ambazo zilitolewa kwa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA)
na mfadhili ,Raia wa Oman kwa ajili ya wananchi wa Zinga.
"Tangu
fedha zilipotolewa visima havikuchimbwa hivyo tulipata taarifa
tulifuatilia na kuhakikisha hazifanyiwi ubadhirifu na kuchimba visima"
Suzan
anaongoza ,kuwa licha ya hayo Mkuranga waliweza kuokoa milioni 21.790
ambazo wakulima walidhulumiwa na viongozi wa bodi za AMCOS za
Njopeka,Chungulo,Njianne na Tunduni Magawa.
Akizungumzia
fedha zilizorejeshwa baada ya kufuatili mikopo iliyotolewa katika
vikundi vya wanawake,vijana na walemavu , alitaja halmashauri ya wilaya
Kibiti ilitoa fedha 550,000 na vikundi hivyo vilishindwa kurejesha .
Fedha nyingine ni milioni 2.600.0 zilizokopeshwa kwa vikundi katika halmashauri ya wilaya ya Rufiji.
Suzan
aliwasihi wananchi kuepuka vitendo vya rushwa kwani dhamira ya Serikali
chini ya Rais Samia Suluhu ni kuhakikisha rushwa inatokomea nchini na
kwamba ubadhirifu na rushwa ni mwiba unaochoma na kuathiri maendeleo na
uchumi wa nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...