Dar es Salaam.  Jumla ya waogeleaji 21 wa klabu ya Taliss wameiwezesha klabu hiyo kushinda jumla ya medali  79 katika mashindano ya Taifa ya kuogelea yaliyomalizika hivi karibuni kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na chama cha kuogelea Tanzania (TSA), kati ya medali 79, kati ya hizo, 35 za dhahabu, 21 za fedha na 23 za shaba.

Mashindano hayo yalishirikisha waogeleaji zaidi ya 90 na Taliss iliibuka na ushindi wa jumla kwa kupata pointi 1,826.

Meneja wa Taliss, Hadija Shebe alisema kuwa matokeo hayo mazuri yametokana na ufundishaji mzuri wa mkocha na mapokeo ya waogeleaji wakati wa ufundishwaji.

“Nawaongeza wazazi, walimu, makocha na wadau wote waliofanikisha timu yetu kushinda ushindi wa  jumla ya kwa upande wa medali, haya ni mafanikio makubwa sana kwa timu na tusibweteke, tunatakiwa kufanya vizuri zaidi,” alisema Hadija.

Kwa mujibu wa matokeo hao, klabu ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC) iliibuka ya pili kwa kupata jumla ya medali 48 ambapo kati ya hizo, 18 ni dhahabu,  18 nyingine ni fedha na 12 za shaba.

Nafasi ya tatu kwa upande wa kushinda medali nyingi imekwenda kwa klabu ya Mwanza iliyoshinda jumla ya medali 36 ambapo  16 za dhahabu, 14  (fedha) na sita za shaba.

Klabu ta nne ni Bluefins ambayo imeshinda jumla ya medali 57 ambapo kati ya hizo, tisa ni za dhahabu, 23 (fedha) na 25 za shaba. Timu nyingine katika orodha hiyo ni FK Blue Marlins iliopata medali 20, ikiwa tisa ni za dhahabu, tano za fedha na sita za shaba.

Timu ya Mis Piranhas ilishika nafasi ya sita kakupata jumla ya medali 14 ambapo tatu za dhahabu, nne za fedha na saba za shaba.

Waogeleaji  wa klabu ya Taliss wakishangilia baada ya kushinda mashindano ya Taifa ya kuogelea yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana, Dar es Salaam.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...