*Wanawake na watoto wa kike wahanga wa ukatili katika mitandao.

*Picha za Udhalilishaji husambazwa wakati kupata nafasi za uongozi na uchaguzi mkuu

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Imeelezwa kuwa ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Wanawake wamekuwa sehemu ya ukatili wa mtandaoni na kufanya baadhi kupoteza maisha na wengine kupoteza mwelekeo baada ya kuona picha zao zisizo na maadili zikizagaa mtandaoni.

Kutokana na mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa Kushirikiana na Friendrich Ebert Stiftung (FES) wamezindua Kampeni maalum ya kupambana na ukatili wa Kijinsia unaofanywa kwa njia ya mitandao ZUMICA#ZuiaUkatiliMtandaoni.

Akizungumza na waandishi wa Habari na wadau Taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na Taasisi za Serikali jijini Dar es Salaam Meneja Mikakati wa TAMWA Sylivia Daulinge amesema kuwa kampeni hiyo ni mwezi Mmoja kuanzia Aprili hadi Juni 6 mwaka huu ikiwa inalenga kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto wa Kike mitandaoni.

"Ilizoeleka kuwa ukatili wa kijinsia unafanywa katika hali ya kudhuru mwili ,kama vile vipigo ubakaji /ulawiti ,utekaji,ndoa za utotoni,mimba za mapema,rushwa ya ngono na matusi"amesema Daulinge

Amesema baada ya kukua Teknolojia ,Ukatili huo sasa unafanyika kwa njia ya mitandaoni ambapo wanawake /wanaume na hata watoto huweza kudhalilishwa kwa namna mbalimbali kwa kutumia mitandao ya Internet kama vile Twitter , Facebook, WhatsApp, Instergram pamoja you tube.

Aidha amesema kuwa Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwa kuna ungezeko kubwa la watumiaji wa Internet ambapo mwaka 2017 watumiaji waliongezeka kwa asilimia 16 na kufikia milioni 23 na asilimia 82 kati yao walitumia mtandao kwa njia ya simu za mkononi huku takwimu katika mitandao Facebook asilimia 38.81, Twitter asilimia 20.95,YouTube asilimia 11.25 na mwisho Instergram asilimia 5.78.

"Tumeona Mara kadhaa video za utupu za Wanawake, Watoto wa kike zikisambazwa katika mitandao hiyo ,Tumeshuhudia matukio ya video za ngononza Wanawake zikisambazwa kwa makusudi kabisa ,huu ni udhalilishaji unafanyika kwa njia ya mtandao "amesema Meneja Mikakati Daulinge.

Amesema baadhi yaa watekelezaji wa uzalilishaji hutumia mitandao ya kijamii kama fimbo ya kuwachapia wanawake na Watoto wa Kike pale wanapofanikiwa katika jambo Fulani au kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi na wakati mwingine Wanawake na Watoto kudhaliloshwa kwa sababu ya wivu mapenzi.

Hata hivyo amesema wakati wa uchaguzi mkuu ukifika nchini picha za Wanawake za udhalilishaji husambazwa kuonyesha hafai kuongeza na hafai kupata nafasi za uongozi anaowania.

Mrakikibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kitengo cha Dawati la Jinsia Leah Mbunda amesema kuwa wamekuwa na matukio hayo na wamekuwa wakiwakamata wahalifu na kuwafikisha mahakamani.

Amesema kuwa katika matukio hayo Wanawake wanaathirika kisakolojia.

Nae Afisa Miradi wa Friedrich Ebert Dtiftung (FES) Anna Mbise amesema kuwa Kampeni hiyo itafanyika kwa mwezi mmoja ila itakuwa endelevu katika utoaji elimu.

Meneja Mikakati wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Sylivia Daulinge akizungumza na  waandishi Habari kuhusiana na Uzinduzi wa Kampeni ya Zuia Ukatili Mtandaoni uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 Imeelezwa kuwa ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Wanawake wamekuwa sehemu ya ukatili wa mtandaoni na kufanya baadhi kupoteza maisha na wengine kupoteza mwelekeo baada ya kuona picha zao zisizo na maadili zikizagaa mtandaoni.

Kutokana na mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa Kushirikiana na Friendrich Ebert Stiftung (FES) wamezindua Kampeni maalum ya kupambana na ukatili wa Kijinsia unaofanywa kwa njia ya mitandao ZUMICA#ZuiaUkatiliMtandaoni.

Akizungumza na waandishi wa Habari na wadau Taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na Taasisi za Serikali jijini Dar es Salaam Meneja Mikakati wa TAMWA Sylivia Daulinge amesema kuwa kampeni hiyo ni mwezi Mmoja kuanzia Aprili hadi Juni 6 mwaka huu ikiwa inalenga kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto wa Kike mitandaoni.

Afisa wa Wizara Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Casmir Ndambalilo akizungumza kuhusiana na Sekta ya Habari katika uzinduzi wa Kampeni ya Zuia Ukatili Mtandaoni.

Picha ya Pamoja ya waandishi na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa kampeni ya Zuia Ukatili Mtandaoni uliofanyika ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...