Jane Edward, Michuzi TV, Àrusha

Wawekezaji wazawa wa viwanda katika Mkoa wa Arusha,wamesimamisha kwa muda Huduma ya uzalishaji kwaajili ya kumuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,Hayati Dr John Pombe Magufuli,ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika sekta ya viwanda.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda kinacho zalisha Transfoma hapa nchini Bwn Zahir Salehe anasema Hayati Magufuli atakumbukwa kwa mengi aliyotendea nchi hii hususani kuwajali watu wa rika zote, Dini zote, bila kujali jinsia.

Amesema kuwa, kiwanda hicho kimeamua kusimamisha uzalishaji kwa muda wa lisaa limoja kukumbuka aliyoyafanya katika sekta ya viwanda pamoja na mambo Mengine bado Watanzania na wamiliki wa viwanda wataendelea kuuenzi mchango wake hapa nchini.

"Tunaweza kuzungumza mengi katika kumuenzi Hayati Magufuli katika kipindi chake cha utawala,sisi wadau wa viwanda katika ulipaji kodi pamoja na wadau wa sekta zingine,tumeweza kuwezesha kufikia uchumi wa kati"Alisema Zahir

Hata hivyo amempongeza Rais wa sita Samia Suluhu Hassan,kwa kufanya mabadiliko katika wizara zake, na kwamba wao kama sekta ya viwanda wameahidi kumpa ushirikiano mkubwa katika kuipeleka mbali nchi ya Tanzania kimaendeleo.

Baadhi yao wafanyakazi wa kiwanda hicho Gabriel Mkenda, wamesema kuwa wanatambua mchango wa Hayati Magufuli na kwamba uwepo wa mama Samia unawapa Hari zaidi ya kuendelea kufanya uzalishaji katika kiwanda hicho na kwamba wana imani kubwa na Rais  Samia ya kuwafikisha nchi ya Ahadi .

Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Transfoma (Tanalec)Zahir Salehe, kushoto ni Michael Mangowi, wakikagua moja ya Transfoma inayozalishwa na kiwanda hicho (Picha na Jane Edward, Michuzi TV, Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...