Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na waumini ya dini ya kiislamu, kwenye Msikiti wa Gaddafi,
jijini Dodoma, baada ya kushiriki sala ya ijumaa, Aprili 2, 2021. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza mawaidha yaliyokua yakitolewa na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Alhajj Mustafa Rajab kwenye Msikiti wa Gaddafi, jijini Dodoma, wakati aliposhiriki sala ya ijumaa, Aprili 2, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Alhajj Mustafa Rajab, wakati aliposhiriki sala ya ijumaa, kwenye Msikiti wa Gaddafi, jijini Dodoma, Aprili 2, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
**********************************
RAIS Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Watazania
waendeleze utamaduni wao uliodumu kwa muda mrefu wa kushikamana,
kupendana na kushirikiana ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa ya amani
na utulivu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili
2, 2021) baada ya sala ya Ijumaa katika msikiti wa Gaddaf jijini Dodoma.
Waziri Mkuu alikuwa akiwasilisha salamu za Rais Mheshimiwa Samia kwa
Watanzania.
Amesema Mheshimiwa Rais Samia anamatumaini makubwa na Watanzania
wote hivyo amewataka waendelee kuwa watulivu na washiriki katika
shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo yao na Taifa kwa
ujumla.
“Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anamatumaini makubwa
kwa Watanzania wote, tuendelee kuliombea Taifa letu na kila mmoja
ashiriki katika shughuli za maendeleo na hatua tunayotarajia itafikishwa
na sisi wenyewe na tukizingatia haya tutafanikiwa sana.”
“Serikali inaendelea na kazi na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa
ofisi mpya za kudumu za Wizara kwa sababu zilizopo zilikuwa za muda tu.
Mkakati wa muendelezo wa kuifanya Dodoma kuwa makao makuu unaendelea.”
Amesema Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha wananchi
wanaendelea kuhudumiwa na kutumikiwa huko huko walipo. “ Serikali ipo
imara na imejipanga vizuri kuwahudumia na hakuna kitakachoharibika
Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao, yote yaliyopangwa
yataendelezwa.”
Akizungumzia kuhusu miradi mkubwa ya kimkakati inayoendelea
kutekelezwa nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali chini ya uongozi wa
Rais Mama Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri kuhakikisha miradi yote
inaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa,
Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania
wamuombee kwa Mwenyezi Mungu Rais pamoja na wasaidizi wake wote ili
waendelee kutimiza majukumu yao ya kuhakikisha wananchi wanapata
maendeleo yanatimia.
“Tumeanza vizuri, tutaendelea vizuri na tutamaliza vizuri,
wananchi tuendelee kumuombea rais wetu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu
aendeee kuwa na afya njema ili atekeleze malengo ya kuwatumikia
Watanzania na hakuna kitakachoharibika.”
Kadhalika Waziri Mkuu ameedelea kuwasisitiza wazazi na walezi
nchini kuhakikisha wanawajengea watoto wao msingi wa kufanya ibada kwa
kuongozana nao kwenye nyumba za ibada kwa kuwa dini zinanafasi kubwa ya
kuwakuza katika maadili mema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...