Na Mwaandishi Wetu Mtwara

SHIRIKA la umeme Mkoani Mtwara (TANESCO) limekutana na kufanya mazungumzo na viongozi, watendaji na madiwani wa kata zinazopakana na bahari kujadiliana jinsi ya kulinda miundombinu ya umeme katika maeneo yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo tuhuma kwa baadhi wananchi wa vijiji vinavyopakana na bahari kuhusika katika kukata nyaya za kushikilia nguzo za umeme katika maeneo yao na kwenda kuvulia samaki ya pweza.

Kikao hicho kilifanyika katika kata ya Mgao halmashauri ya Mtwara ambapo viongozi hao pamoja TANESCO walikubaliana kuwa na ushirikiano katika kulinda mindombinu ya umeme.

Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja wa shirika la TANESCO Jumanne Nkunguu aliwaambia viongozi wa maeneo hayo kuwa TANESCO ni shirika la umma ambalo huwa ni pamoja na wananchi hivyo viongozi wa vijiji, watendaji na madiwani wanatakiwa kuwahimiza wananchi wao kulinda miundombinu kwa faida ya yao na taifa.

Amesema kumekuwepo na shida ya kukatikatia umeme kutokana na uharibifu wa miundombinu ya umeme ikiwemo kukakatwa kwa nyaya za kushikilia nguzo za umeme, kuchoma moto miundommbinu ya umeme.

Nkunguu aliwaambia viongozi hao kuweka kuhakikisha wananchi wao wanalinda miundombinu ya umeme kwan serikali inatumia gharama nyingi kuwafikishia huduma ya nishati katika maeneo yao.

Amewataka viongozi wao kuwaeleza na kuwajibisha wale wote wanaohusika na uharibu wa miundombinu ya umeme katika maeneo yao. Amesema wananchi hao wamekuwa wakiharibu mpaka transfoma ya umeme na kusababisha hasara kubwa kwa serikali.

“Kwanza wananchi wengine wanakosa huduma ya umeme katika maeneo yao na kusababisha hasara kwa serikali kwa sababu transfoma moja ni 25m/- …ni gharama kubwa sana kuanza kununua trasfoma mpya kwa ajili ya kuharibiwa na wananchi wasiojali,” amesema.

Kwa upande wao, viongozi hao waliliomba shirika hilo kuandaa mafunzo ya mara kwa mara kuelimisha wananchi umuhimu wa uwepo wa miundombinu hiyo ya umeme katika maeneo yao.

“Sisi tunalinda mali hizi, lakini wapo wananchi ambao hawajui umuhimu au madhara ya kuharibu hizo nyaya na hata mtu akiona mwenzake anaharibu hawezi kustuka wala kuchukua hatua yoyote kwa sababu hawajui hata sheria ya kuharibi mali ya umma inasemaje,” amesema Diwani wa Kata ya Naumbu Halmashauri ya Wilya ya Mtwara Rashidi Abderehemana.

Ametowa wito kwa TANESCO kwenda kuwaelimisha wananchi hao pamoja na viongozi wa vijiji na kata sheria za kulinda miundombinu, adhabu za kuharibu mali ya umma na madadhara ya kuharibu miundombinu ya umeme katika maeneo yao.

Afisa Uhusiano wa Huduma Kwa Wateja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mkoani Mtwara Jumanne Nkunguu akizungumza na wenyeviti na watendaji wa Vijiji Kata ya Naumbu kuhusu kushirikiana kulinda miundombinu ya umeme katika maeneo Yao.
Sehem ya wenyeviti na watendaji wa Kata ya Naumbu Halmashuri ya Wilaya ya Mtwara wakimsikiliza Afisa Uhusiano Kwa Wateja Jumanne Nkunguu kuhusu kushirikiana katika kulinda miundombinu ya umeme. Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo shtuma za wananchi wa Vijiji vinavyozunguka bahari kukata nyaya za umeme zinazoshikilia nguzo za umeme na kwenda kuvulia samaki aina ya pweza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...