Na Richard Mwamakafu, Dodoma
Serikali
ya Tanzania na Indonesia zimekusudia kukuza ushirikiano katika sekta ya
Utamaduni wa Utalii ili kuongeza ajira kwa vijana wa mataifa yote
mawili.
Haya yamebainika Jijini Dodoma baada Mheshimiwa.
Innocent Bashungwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
kukutana Aprili 23, 2021 na kufanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia
Nchini Prof. Ratra Pardede.
Katika mazungumzo hayo serikali ya
Tanzania imemwomba Balozi huyo kuunga mkono jitihada za kukuza Sanaa
nchini kwa kuchangia katika uwekezaji wa Vifaa vya kuzalishia Filamu na
kwakuanzisha Maktaba ambayo itakuwa chini ya Uangalizi wa Chuo na kwa
Usimamizi wa Serikali ili kukiendeleza Chuo cha Bagamoyo TASUBA
”Tukiwekeza
katika vijana wa sasa tunajenga Taifa imara la kesho na Viongozi bora
ambao watakuwa Mabalozi wazuri katika Maendeleo ya Nchi zetu Mbili,
Ukizingatia Indonesia ni kati ya Nchi zinanokuwa Kiuchumi na kwa kasi
sana Duniani. Jambo hili linaweza likaitoa Tanzania katika Uchumi wa
Kati na Kukua zaidi.” Alilisisitiza Waziri Bashungwa.
Mazungumzo
hayo yalienda mbali zaidi kwa kusema hatua hii itasaidia Ukuaji wa
Sanaa za Filamu Nchini na kuutangaza utamaduni wetu na kuvutia utalii
kwa ujumla utakao inua pato la nchi na kuwawezesha vijana ambao ni
watashika nyadhifa mbalimbali hapo baadae.
Prof.Pardede
alishukuru kwa mazungumzo hayo pia akakili kuvutiwa sana na Utamaduni wa
Kitanzania ambao ni kivutio kikubwa sana kwa Taifa la Indonesia.
“Ninatoa
mwaliko kwa Waziri Bashungwa Kuhudhulia Tamasha la Utamaduni wa
Kindoneshia litakalofanyika Mei 29, 2021 Jijini Dar es Salaam Tanzania
ambalo litavijumlisha vikundi mbali mbali vya Kitamaduni vya Nje na
ndani ya Nchi ambalo limelenga hasa kuinua Utalii wa Sanaa na Chakula
baina ya Tanzania na Indoneshia.” Alisema Balozi huyo
Mazungumzo
haya yanakuja baada ya kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania juu ya Secta ya Sanaa kutoa ajira zaidi kwa vijana wengi
Nchini.
Hadi sasa Nchi ya Indoneshia imetoa nafasi za Ufadhili
kwa vikundi vya Sanaa na Utamaduni Nchini kukutana na Wasanii mbalimbali
kutoka Nchini Indoneshia ili kubadilishana Ujuzi wa Sanaa na
kujiongezea ujuzi binafsi kwa kipindi cha Miezi Sita Nchini Indonesia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...