Na Woinde Shizza, ARUSHA
CHAMA cha wafanyabiashara mkoa wa Arusha (TCCIA) kimeanza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa nyama katika jiji la Arusha, namna ya kuendesha biashara hiyo kwa kufuata Sheria na kuzingatia kanuni ya biashara hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari Katika warsha hiyo mwezeshaji wa TCCIA, Charles Makoi amesema kwamba TCCIA imelazimika kuwawezesha wafanyabiasha hao kupata mafunzo ambayo yatasaidia kuondoa mkanganyiko na mamlaka za Nyama kwa kutambua Sheria za bodi ya nyama.

Amesema TCCIA inatamani kuona wafanyabiashara wa nyama Mkoani hapa wanafanya kazi zao katika mazingira Safi na salama kwa kufuata sheria na kama kuna maeneo wanavuka mipaka basi bodi ya nyama iweze kuwapa maelezo na taratibu za kufuata kufanya kazi kwa urais

"Mafunzo haya yanaendeshwa na maofisa wa bodi ya Nyama lengo ni kuona namna ya kuondoa matatizo Kati ya wadau wa nyama na Bodi ya Nyama." Amesema

Aidha ameitaka bodi ya Nyama nchini kusogeza huduma zake kwa kufungua ofisi Katika mkoa wa Arusha ili kuwezesha wafanyabiashara wa Nyama kutambua mapema mabadiliko ya sheria za nyama.

"Tumepokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara wa Nyama na wakilalamikia mabadiliko mengi ya sheria ya Nyama hivyo tumeona tuwakutanishe na bodi ya nyama waweze kujadili kwa pamoja na kuweka mikakati ya uendeshaji biashara." Amesema Makoi

Awali akiendesha warsha hiyo Afisa Nyama kutoka bodi ya Nyama Tanzania, Edgar Mamboi amesema miongoni mwa changamoto walizogundua kwa wadau wa Nyama ni ukosefu wa Elimu ya Nyama na Masoko pamoja na ukosefu wa mifugo Bora ya Nyama.

Amesema kuwa bodi ya Nyama imejipanga kuimarisha mifumo ya biashara ya Nyama nchini, usajiri, masoko na Mawasiliano ili kuwa karibu na wafanyabiashara wa Nyama ikiwemo kuwasogezea huduma kwa kufungua ofisi za kanda na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata Nyama.

Matatizo mengine ni ukosefu wa mifugo pamoja na bei ambazo zimekua sio rasmi hivyo kupeleka kuyumba kwa masoko ya nyama hivyo wao kama bodi wameyapokea na kwenda kufanya kazi mapema hili kunusuru sekta hiyo kupoteza mapato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...