Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeondoa zuio kwa "Freelancers" Mawakala wa Mitaani ambao walizuiwa kutoa huduma za usajili wa kadi za Simu (Line) kwa kutumia alama za vidole.

Mnamo Februari 16 mwaka huu TCRA ilitoa maelekezo ya kusitisha shughuli za Freelancers katika usajili wa laini za simu kibayometria ifikapo May, 2021 na badala yake ikaagizwa usajili ufanyike katika maduka maalum au mahali maalum kwa mujibu wa kanuni za usajili wa laini za simu 2020.

"TCRA imeondoa zuio kwa watoa huduma na wanaweza kuendelea kuwatumia Freelancers bila kuathiri usajili sahihi wa laini za simu kibayometria wakati inafanya tathmini upya ya namna bora inayoweza kutumiwa na watoa huduma kuwasimamia Freelancers", Mkurugenzi Mkuu wa TCRA  Dkt Jabir Bakari Kuwe (pichani) katika taarifa yake iliyosambazwa kwa vyombo vya habari akiwa  Makao Makuu ya Mamlaka hiyo mkoani Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...