KUTOKA ARUSHA

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameipongeza Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya Mkoa wa Arusha (RHMT) kwa kufuatilia changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi na Watoto wachanga kwa kuanzisha kanzi data ikiwa ni mkakati wa kupunguza vifo hivyo kwa mwaka 2021-2023.

Dkt.Gwajima amesema hayo Leo wakati aliongea na timu hiyo Kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha

"Niwapongeza sana timu  hii kwa ubunifu huu wa kuanzisha mkakati wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na Watoto wachanga  kwa kutumia kanzi data ya ufuatiliaji wajawazito wanaolazwa chumba Cha kujifungulia.

Aidha, Dkt. Gwajima ameipongeza Timu ya Uendeshaji  Huduma za Afya Wilaya ya Arusha (CHMT) kwa kusimamia mapato vituoni wao wenyewe Hali iliyopekekea kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato Kwenye vituo vya afya vya Wilaya hiyo.

Pia Dkt. Gwajima ameipongeza kamati hizo kwa ushirikiano na uwajibikaji wa pamoja   na hivyo kupelekea kumtoa Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa
n.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...