Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania, na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, zimempongeza rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan, sio tuu kwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali pia kwa kuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mwanamke, ambapo urais wa Samia, umeipaisha  nafasi ya Tanzania, kitaifa na kimataifa katika safari ya kuelekea kwenye usawa wa kijinsia kwenye uongozi wa kisiasa.

 

Pongezi hizo zimetolewa jana na Mkurugenzi wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total nchini Tanzania, (Total Network Director) , Bi Marieme Sow, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini.

 

Marieme Sow amesema, kitendo cha Mama Samia kuwa rais wa kwanza mwanamke kwa Tanzania, na kwa nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki na rais kamili wa 4 barani Afrika, urais wa Samia umeipaisha sana Tanzania  katika anga la kimataifa, katika kuthibitisha Tanzania imepiga hatua kubwa kuelekea kwenye usawa wa kijinsia, na sio tuu kuthibitisha mwanamke ana uwezo sawa na mwanaume, bali kuthibitisha kuna wanawake wana uwezo kuzidi hata wanaume ila wamekuwa wanakosa fursa  sawa kwa sababu tuu, wao ni wanawake, Rais Samia ni uthibitisho wa uwezo wa mwanamke, “the power of a Woman”

 

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total Tanzania, Marsha Msuya Kilewo, amesema Total Tanzania inaamini uwezo wa  wanawake na kuthamini mchango wa wanawake kwa maendeleo ya taifa, ndio maana imejiunga na Taasisi ya Flaviana Matata, kuunga mkono juhudi zozote za kuwajengea uwezo sawa watoto wa kike, na kwa kufanya kampeni ya mwezi mzima, ukijaza mafuta  kituo chochote cha Total Tanzania, unakuwa umesaidia kuchangia maendeleo ya wanawanake wa Tanzania.

 

Kwa upande wake, Flaviana Matata, aliishukuru kampuni ya mafuta ya Total kwa kuunga mkono kampeni yake kuwajali watoto wa kike na kusema, “Ukimsaidia mtoto wa kike, ni umeisaidia kumtengeneza Samia mwingine, na kuwasisitizia wanafunzi hao wa Jangwani, kusoma kwa bidii, ili Tanzania tuweze kupata akina Mama Samia wengi zaidi katika sekta zote”

 

Mwakilishi wa Mamlaka ya Elimu nchini TEA, Hamza Hassan, aliipongeza Total Tanzania na Flaviana Matata Foundation, kusaidia watoto wa kike mashuleni, na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo kwasababu bado mashule yanakabiliwa na changamoto mbalimbali.

 

Kaimu Mkuu wa shule ya Jangwani, Mwalimu, Paulina Aweda, aliishukuru Total Tanzania na Flaviana Matata Foundation, kusaidia shule yao, na kusisitiza msaa huo ni muhimu sana, na sio kwa watoto tuu wa familia masikini, lakini hali hiyo huweza kumtokea mwanafunzi mwingine wakati wowote akiwa hakujiandaa, na kuharibu concentration yake kwa kukosa confidence na kuwaza atafanyafanyaje,  hivyo msaa huo unarejesha tabasamu la mtoto wa kike kusoma kwa uhuru wakati wote bila wasiwasi wowote.

 

Mwalimu alitumia fursa hiyo, kuendelea kuomba misaa kwa jamii, kufuatia shule ya Jangwani kupokea wanafunzi wenye mahitaji maalum ya ulemavu wa viungo, wanafunzi hao wenye mahitaji maalum, bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohiji jamii kuwasaidia, hivyo aliomba taasisi nyingine ziinge mfano wa Total Tanzania katika kusaidia jamii.

 

Wanafunzi waliogawia taulo hizo, nao walishukuru kwa furaha, na kuahidi kusoma kwa bidii na wao kuja kuwa kama Mama Samia.

Mkurugenzi wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total nchini Tanzania, (Total Network Director) , Bi Marieme Sow,  (aliyekaa mbele ya mti) akiwa amejichanganya na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total nchini Tanzania, (Total Network Director) , Bi Marieme Sow,  (anayeonekana kwa nyuma) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total nchini Tanzania, (Total Network Director) , Bi Marieme Sow, (Mwenye gauni jeupe), akiwa na Mwanamitindo, Flaviana Matata, ( katikati) na Ofisa mawasilano wa Total, Zoe Okoedion (Kushoto) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total Tanzania, Marsha Msuya Kilewo, akigawa taulo za kike kwa mwanafunzi wa Jangwani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki.

Mwana mitindo Flaviana Matata, akimsaidia mwanafunzi wa Jangwani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki

Wafanyakazi wa Total Tanzania na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation katika picha ya pamoja na waalimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani  wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki

Wafanyakazi wa Total Tanzania na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation katika picha ya pamoja na waalimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani  wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani  wakifurahia kugaiwa bure taulo za kike, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani  wakifurahia kugaiwa bure taulo za kike, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, ambapo Total Tanzania, imechangia ununuzi wa taulo hizo na kuzigawa bure kwa wanafunzii wahitaji kutoka familia masikini katika kuwasaidia kuwa sawa na wanawake wengine wote kwasababu wanawake wote, wanamahitaji sawa bila kujali uwezo, utajiri au umasikini. Tukio hili limefanyika mwishoni mwa wiki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...