Na Muhidin Amri,Songea
WAFANYABIASHARA wadogo na wakubwa mkoani Ruvuma,wametakiwa kusajili
biashara zao ili ziweze kutambulika kisheria na kufungua wigo
utakaosaidia kupata wateja wengi na mikopo kutoka katika taasisi za
fedha.
Hayo yamesemwa jana na Afisa Msajili msaidizi wa Wakala wa usajili wa
biashara na leseni(Brela) Swalehe Yahaya wakati akitoa elimu juu ya
usajili wa majina ya biashara na makampuni kwa
wafanyabiashara,wasindikaji chakula na watengenezaji bidhaa ndogo ndogo
wa Manispaa ya Songea katika ukumbi wa Sido mjini Songea.
Alisema,elimu hiyo itawasaidia wafanyabiasha namna bora ya kusajili
biashara zao,kujitangaza,kukuza na kulinda majina ya biashara zao ili
kuepuka kuingiliwa na watu wengine.
Alitaja faida nyingine ya kusajili biashara inamwezesha kuomba zabuni
kwenye taasisi za umma ambapo kutokana na sheria mpya ni vigumu kwa
mfanya biashara asiyesajili biashara au kampuni yake kupata zabuni
serikalini.
Baadhi ya wafanya biashara wamepongeza hatua ya Brela kutoa elimu hiyo
kwani imefungua fursa ambayo itatangaza shughuli wanazofanya na uhakika
wa kuuza bidhaa zao katika masoko mbalimbali ya ndani nan je ya mkoa wa
Ruvuma.
Belinda Lyimo, ameishukuru Brela kuendesha mafunzo na kutoa elimu
ambayo inakwenda kuwahamasisha kutengeneza bidhaa bora zenye uwezo wa
kumudu kwenye soko la ushindani kuongeza idadi ya wateja ikilinganisha
na apo awali ambapo licha ya kuzalisha bidhaa bora, lakini
hazikutambulika na watu wengi.
Ambinga Swai alisema,elimu ya usajili wa biashara na makampuni
iliyotolewa na Brela itawezesha wafanya biashara sio kutambulika tu bali
hata kulinda majina yao yasitumiwe na watu wengine kujinufaisha.
Alisema, ni jambo jema kwa wajasiriamali na wafanya biashara kuweka
mambo yao kisheria ili kulinda biashara zao,kuongeza idadi ya wateja na
uhakika wa kupata zabuni kutoka kwenye taasisi za serikali.
Amewata wafanyabiashara, kuepuka kufanya shughuli zao kwa mazoea kwani
tabia hiyo ndiyo inayo changia sana kurudisha nyuma juhudi zao licha ya
kuzalisha na kuuza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.
Katibu Tawala msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoa wa Ruvuma Deogratius Sibula kushoto akimkabidhi cheti cha usajili wa Biashara mjasilimali mdogo Belinda Lyimo wakati wa mafunzo ya utoaji elimu ya usajili ya Biashara na makampuni yaliyotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara,leseni na Makampuni Brela yaliyofanyika jana mjini Songea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...