Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wakulima
wa zao la chai hapa nchini wametakiwa kujengewa uwezo juu uzalishaji wa
zao hilo na kuongeza thamani ili liweze kupata masoko ndani na nje ya
nchi.
Kauli hiyo
imetolewa na mratibu wa mradi wa Markup Tanzania Safari Fungo katika
kikao cha kuwajengea uwezo wadau wa chai nchini kilichofanyika hapa
mkoani Njombe.
Amesema
wazalishaji wa zao la chai wanapaswa kupatiwa mbinu na kujengewa uwezo
kuanzia wakati wa kuvuna, kuongeza thamani pamoja na namna ya kupata
masoko ndani na nje ya nchi.
Amesema
ili wakulima na wazalishaji wafanikiwe wanapaswa kupatiwa mafunzo ya
nadharia kwa kujengewa uwezo darasani na baadae shambani kuona namna
mafunzo waliyoyapata wanavyoweza kuyabadili katika vitendo.
Amesema
mafunzo hayo yanaweza kufanikiwa na kuinua viwango vya ubora endapo
wadau wa zao hilo wakiwemo viongozi kutoka serikalini na wazalishaji wa
zao hilo wadogo, wakati na wakubwa watashirikiana.
Amesema
hilo likifanyika zao hilo la chai kutoka Tanzania litaweza kupata
masoko kuanzia ndani ya nchi na nje ya nchi hususani barani ulaya ambalo
ndiyo wadhamini wa mradi huo.
"Ninaamini
kupitia zoezi hili wakulima na wafanyabiashara watahakikisha mambo haya
wanakwenda kuyatekeleza kwenye biashara zao" amesema Safari.
Ofisa
kutoka wizara ya kilimo makao makuu idara ya maendeleo ya mazao na
masoko ya kilimo Fikiri Katiko amesema kupitia mradi huo wa Markup
kupitia ITC katika kuongeza thamani ya zao la chai ni moja ya kipaumbele
cha serikali kwenye zao hilo.
Amesema
serikali imeweka maeneo muhimu manne katika kukuza na kuboresha mazao
ya kimkakati ambayo ni pamoja na matumizi bora ya maji na ardhi,
kuongeza uzalishaji na tija, kuongeza thamani ya masoko.ya mazao na
kuweka mazingira bora ya kufanya biashara.
Amesema
katika zao la chai kwa wastani uzalishaji ni tani elfu thelathini kwa
mwaka ambapo asililimia thelathini ni wakulima wadogo na zilizosalia ni
wakulima wakubwa.
"Katika
chai kavu asilimia 85 inakwenda kuuzwa nje ya nchi na 15 inatumika
ndani ya nchi kwenye viwanda vyetu kwa ajili ya kutengeneza majani ya
chai" amesema Fikiri.
Meneja
mkuu wa kiwanda cha chai Ikanga Gerald Ngenzi amesema sekta chai
nchini inapitia wakati mgumu tofauti na miaka mitano iliyopita
changamoto kubwa ikiwa kwenye suala la bei.
Amesema
zao la chai kama ilivyo kwa mazao mengine ni lazima liweze kushindana
kimataifa lakini ili lifanikiwe katika ushindani huo lazima zao hilo
liwe na ubora.
"Kupitia
Markup wataalam mbalimbali wanafundishwa, kuwezeshwa ili kuhakikisha
wanarudi shambani kutekeleza mafunzo waliyoyapata ili mkulima azalishe
chai iliyo bora" amesema Gerald.
Baadhi
ya wakulima walioshiriki kikao hicho cha wadau wa chai akiwemo Kennedy
Peter kutoka wilaya ya Tarime mkoani Mara amesema kuanzishwa kwa soko
la mnada wa chai hapa nchi utawawezesha wakulima kupata bei nzuri
itakayosaidia kuboresha maisha yao.
Amesema
vile vile kupitia mnada huo utakaokuwa hapa nchini taifa litanufaika
kwa kupata fedha za kigeni ambazo zitasaidia kuimarisha uchumi wa nchi.
"Vijana
wengi hawajikiti katika zao hili kwasababu ya ugumu wake kwenye bei
pamoja na masoko hivyo serikali inapaswa kuweka viwanda ili kuinua
thamani ya zao .la chai" amesema Kenedy.
Mratibu wa mradi wa Markup Tanzania Safari Fungo akieleza namna
wakulima wanavyopaswa kujenhgewa uwezo ili kutoa mazao bora
yatakayoingia katika soko la kimataifa.Baadhi
ya wadau wa zao la chai wakiwemo wakulima na wasimamizi wa viwanda vya
chai wakisikiliza semina iliyokuwa inatolewa mkoani Njombe kwa wadau
hao.
Mmoja wataalamu akitoa mafunzo kwa wadau wa chai juu ya kilimo cha chai na ubora wa zao hilo unaotakiwa sokoni.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...