Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

SERIKALI imewahakikishia wawekezaji kuwa wasisite kuwaajiri watanzania kwa kuwa wanaajirika, wachapa kazi,waadilifu na waaminifu kwa kiasi kikubwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA Assemblers kilichopo Kibaha mkoani Pwani ambapo uongozi wa kiwanda hicho umethibitisha uadilifu na uaminifu wa vijana wafanyakazi wa Tanzania.

"Uongozi wa kiwanda hiki umethibitisha tabia njema na weledi wa watanzania, hakuna wizi na nikuhakikishie Mkurugenzi watanzania wanaajirika, wafanyakazi na waaminifu na niwaombe wafanyakazi wa kiwanda hiki na maeneo mengine endeleeni kuwa mabalozi bora kwa nchi yetu." Amesema.

Majaliwa amesema, kiwanda hicho cha kuunganisha magari ya mizigo mizito na kati kimeonesha wazi dhamira yake kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika azma yake ya ujenzi wa viwanda.

"Katika uwekezaji wa bilioni 12 wa GFA Assemblers tayari asilimia 48 umefikiwa na Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada hizi kwa kuongeza maeneo zaidi ili muendelee kuwekeza zaidi katika uunganishaji wa magari mengine yakiwemo ya abiria na binafsi." Amesema.

Aidha amemtaka mwekezaji wa kiwanda hicho kuwa balozi katika nchi yake kwa kuwaalika wawekezaji wengi zaidi kwa kuwa Tanzania ni nchi sahihi na yenye sera sahihi kwa wawekezaji.

Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho Aljawad Karimal amesema, kiwanda hicho kinaunganisha magari (malori mepesi,) kitaifa na Kimataifa.

"GFA ilianza kufanya kazi mwezi wa 9 kwa uwekezaji wa bilioni 12 na hadi sasa tumefikia uwekezaji wa bilioni 4 na tumefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 100, kuongeza pato la taifa pamoja na wazawa kupata Teknolojia kutoka nje." Amesema.

Karimal ameiomba Serikali kutoa vipaumbele kwa sekta binafsi hasa katika masoko kwa taasisi na Halmashauri kwa kukiangalia kiwanda hicho ambacho kinaunganisha magari ya taka, maji safi na maji taka, magari ya ulinzi, afya, usalama, usafirishaji na mwendokasi." Amesema.

Pia ameiomba Serikali kupitia sera zake kuyaangalia makampuni binafsi ya ujenzi, usafirishaji na madini kwa kuwapa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kukuza sekta za ndani.

Aidha ameieleza changamoto ya upatikanaji mdogo wa umeme unaoukabili kiwanda hicho hoja iliyojibiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO,) MKoa wa Pwani Mhandisi. Mahawa Mkaka aliyeeleza kuwa laini mbili za umeme wa viwanda unajengwa pamoja na mradi wa Mloganzila hadi Maili Moja zitakidhi mahitaji ya wawekezaji wa Mkoa huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikabidhiwa nembo ya Kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA Vehincle Assembly na Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Ally Jawad,kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani. Aprili 19,2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA Vehincle Assembly kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani, Aprili 19,2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA Vehincle Assembly  Mkuu Ally Jawad kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani. Aprili 19,2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mageti ya kielektroniki katika kituo cha mabasi ya mwendokasi, gerezani Kariakoo alipototembelea kuona utendaji kazi wa Shirika la Dart. Aprili 19,2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


aziri Mkuu Kassim Majaliwa akitia saini katika moja ya gari liliunganishwa na kiwanda GFA Vehincle Assembly kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani. Aprili 19,2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...