Na Jusline Marco-Arusha

Serikali kupitia wizara ya afya  inatarajia kuzindua utekelezaji wa afya ya kupambana na ugonjwa wa malaria nchini kwa kuanzisha upimaji wa malaria kwa wananchi katika kaya ikiwa ni pamoja na kuandaa mkakati wa kupunguza ugonjwa huo hadi kufikia chini ya asilimia 3.5 kwa mwaka 2021/2025.

Akifunga mkutano wa waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya malaria duniani Dkt.Samwel Lazaro Naibu Meneja mpango wa kudthibiti malaria alisema kuwa Afua hiyo itazinduliwa na waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee ma watoto Dkt.Doroth Ngwajima.

Aidha Dkt.Samwel alisema Mikoa itakayoanza na utekelezaji wa AFUA  hiyo kwa awamu ya kwanza ni Mkoa wa Arusha, kilimanjaro na Manyara ambapo mwaka ujao wataongeza Mkoa wa Njombe na mwaka 2023 na Mkoa mwingine wa Iringa.

"Afua hii mpya inalenga kuhakikisha mikoa hii mitano inafikia kiwango cha maambukizi ya malaria kwa asilimia 0 ifikapo mwaka 2025 ambapo katika utelelezaji wake itakuwa  ni kupima watu katika kaya  ambapo kitakachofanyika ni mgonjwa atakapogundulika ana malaria atakapoenda kupima katika kituo cha kutolea hutuma basi kutakuwa na ufuatiliaji katika ngazi ya kaya kwa wanakaya wote kupimwa ili kutibu na kuzuia kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huo," Alieleza Dkt Samwel.

"Pia ikigundulika kuwa kunamazalia au chanzo cha mbu katika jamii hiyo kutakuwa na afua nyingine ya kuhakikisha hayomazalia aidha ni madimwi yatapigwa dawa ili kuua mazalia hayo na mwisho wa siku ile jamii tutakuwa tumeikinga na maambukizi ya malaria," Alifafanua.

Aliiomba jamii kushiriki kikamilifu kuhakikisha wanautokomeza ujonjwa wa malaria katika mikoa hiyo ifikapo mwaka 2025 ambapo mpango huo unawataka kupunguza malaria kufikia chini ya asilimia 3.5 kama nchi kwenye mikoa 5 ambayo iko chini katika maambukizi ya ugonjwa huo itahusika katika utokomezaji wa malaria kwa miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa ufuatiliaji na tathimini kitengo cha malaria Dkt.Sejenunu Aron alisema kuwa malengo ya Tanzania ni kutokuwa na malaria kabisa ambapo hadi sasa wameweza kupunguza  wingi wa watu wanaopata malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14.8 ya mwaka 2015.

"Sambamba na hayo  idadi ya vifo vitokanavyo na malaria imepungua kwa asilimia 61 huku mikoa ya Kigoma,Geita , Kagera,Mtwara na Ruvuma ikiea na kiwango cha juu ya asilimia 9 ya maambukizi ya Malaria,"Alisema Dkt Sijenunu.

Vilevile alisema kuwa katika Mkoa wa Kigoma maambukizi yapo kwa asilimia 24.4, Geita 17.3, Kagera 15.4, Mtwara 14.8 na Ruvuma 11.8, huku mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya na Songwe maambukizi yakiwa chini ya asilimia 1.

kwa upande wake Charles Mwalimu kutoka wizara ya afya kitengo cha uthibiti wadudu wanaoeneza ugonjwa huo alisema lengo la udhibiti ni kupunguza maambukizi ya malaria kutoka kwa mbu  kwenda kwa binadamu.

"Mikakati yetu ni kuweza kumuua mbu au kumzuia asiweze kumfikia binadamu kwa kuhimiza matumizi ya vyandarua vilivyowekwa viuatilifu vya muda mrefu, unyunyuziaji wa viuatilifu kwenye kuta za nyumba pamoja na udhibiti wa mazalia ya mbu katika mazingira na hizi ni njia zilizoonyesha kuwa na uwezo mkubwa," Alisema.

Naye mkuu wa kitengo cha vipimo, matibabu na dawa kinga za malaria Dkt.Abbdallah Lusasi amesema mpango mkakati wao ni  kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria kwa asilimia 85 kwa makundi hatarishi ya wajawazito na watoto chini ya miaka 5 huku akitaja madhara yayokanayo na ugonjwa huo kwa wajamzito kuwa ni pamoja na kupata upungufu wa damu, mimba kuharibika, kujifungua mtoto njiti pamoja na uwezekano wa kutokea kifo kwa  mama na mtoto.

Naibu Meneja mpango wa kuthibiti malaria Dkt.Samwel Lazaro,akifunga mkutano wa wanahabari kuelekea kilele cha siku ya Malaria Duniani
Charles Mwalimu kutoka wizara ya afya kitengo cha uthibiti wadudu wanaoeneza ugonjwa akieleza hali ya maambuzi ya ugonjwa wa Malaria katika mikoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...