Na Khadija Seif, Michuzi Tv
MWANAMUZIKI Mashuhuri kutoka Congo na Afrika Mashariki - ALICIOS baada ya kutoa albamu yake 2020 na kufanya vizuri katika Mitandao maarufu ya kusikiliza muziki ndani na nje ya Afrika mwezi Mei ameachia Wimbo mpya uitwao “KIMYA” ambao unazungumzia mapenzi kwa namna ya kuridhia na kuyafurahia kiasi cha kuongeza kadri siku zinapozidi kwenda.
Licha ya Mji anaotoka Congo - GOMA kukumbwa na mlipuko wa Volcano katika siku ambayo alitoa wimbo huo, habari njema ni kuwa msanii huyo yupo mbioni kufanya changizo kusaidia wahanga wa volcano. Kwa kirefu zaidi tembelea kwenye account zake za mitandao ya kijamii @alicioscongo
“Kimya imetengenezwa na Mtayarishaji wa muziki kutoka Congo anayeitwa MASTOLA MUSIC, na imeandikwa na Alicios mwenyewe.
Unaweza kuusikiliza kupitia platform zote za kusikiliza muziki duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...