Benki ya Exim imetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwenye vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini Dar es Salaam, Mbeya, Shinyanga na Karatu ikilenga kuwawezesha watoto hao waweze kusherehekea vizuri sikukuu ya Eid El Fitr.
Msaada huo ulikabidhiwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiwa wameambatana na wafanyakazi wengine na ulihusisha mahitaji muhimu ikiwemo mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga wa sembe, unga wa ngano, maharage pamoja na katoni za juisi na maji ya kunywa.
Jijini Dar es Salaam, akiwasilisha msaada huo katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha New Faraja Orphanage Centre kilichopo Mburahati jijini humo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu alisema imekuwa ni utaratibu wa benki hiyo kusaidia makundi na taasisi mbalimbali kupitia ppango wake wa uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaofahamika kwa jina “Exim Cares”.
“…Msaada huu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, na ni mwendelezo wa utaratibu wetu wa kile ambacho tumekuwa tukikifanya kila mwaka ambapo wafanyakazi wa benki ya Exim pamoja na uongozi kwa ujumla tumekuwa tukiguswa kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi kwenye vituo hivi wanafurahia Sikukuu hizi kama wenzao waliopo majumbani,'' alisema.
Bw Kafu alivitaja vituo vingine ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Nuru kilichopo jijini Mbeya, Kituo cha Shinyanga Society for Orphans na kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija vilivyopo mkoani Shinyanga pamoja na Kituo cha Shalom Orphanage and Children Care Centre kilichopo wilayani Karatu.
Zaidi Bw Kafu alitoa wito kwa watoto hao kuhakikisha wanasoma kwa bidii huku wakitanguliza nidhamu kwenye kila jambo wanalofanya ikiwemo masomo na shughuli zao za kila siku wawapo shuleni na kituoni hapo.
“Imekuwa ni furaha kwetu Benki ya Exim kuona kwamba tumekuwa tukipata wafanyakazi na wateja wenye mafanikio makubwa ambao baadhi yao wamepitia katika vituo hivi na kwasasa wanafanya kazi zao kwa bidii na kwa weledi mkubwa. Ili hayo yatimie na kwenu pia ni wajibu wenu kusoma kwa bidii pamoja na kutii maagizo ya walezi wenu kwa nidhamu kubwa,’’ alisema.
Kwa upande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru benki ya Exim kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani huku wakiomba taasisi hiyo na wadau wengine kuendelea kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
“Tunashukuru sana benki ya Exim na wafanyakazi wote kwa kuguswa na kuona umuhimu wa kuesherekea siku hii muhimu na watoto yatima. Tunaomba waendelee kuguswa ili watusaidie zaidi katika kutatua changamoto nyingine ikiwemo suala la bima za afya kwa watoto kwa kuwa baadhi yao hawana bima hizo muhimu.'' alisema Bi Zamda Idrissa Mlezi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim Bw Stanley Kafu (Katikati) akikabidhi msaada ya vyakula na vinywaji kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanage kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani. Msaada wa aina hiyo pia ulitolewa na benki hiyo kwenye mikoa ya Mbeya, Shinyanga na Wilaya ya Karatu.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim Bi Mariam Mwapinga (Katikati) akikabidhi msaada ya vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanage kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Mlezi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Faraja Orphanahe Centre kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam Bi Zamda Idrissa (wa pili kulia) akitoa neno la shukrani kwa benki ya Exim kufuatia msaada huo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Diwani wa Kata ya Makurumla, wilayani Ubungo Bw Bakari Kimwanga (wa kwanza kulia)
Meneja Benki ya Exim tawi la Mbeya Bi Shamsa Shambe (Kushoto) akikabidhi msaada ya vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Madina cha jijini Mbeya Bi Aisha Hamisi ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani
Meneja Benki ya Exim tawi la Mbeya Bi Shamsa Shambe (Kulia) akikabidhi msaada ya vyakula kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru cha jijini Mbeya Bi Mary Kassim ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Baadhi ya wafanyakazi benki ya Exim tawi la Mbeya wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bi Shamsa Shambe (wa pili kulia) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru cha jijini Mbeya mara baada ya kukabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Meneja Benki ya Exim tawi la Shinyanga Bi Sarah Tito (Kushoto) akikabidhi msaada ya vyakula kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Meneja Benki ya Exim tawi la Shinyanga Bi Sarah Tito (wa tatu kulia) akizungumza wakati akikabidhi msaada ya vyakula kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans kilichopo Mkoani Shinyanga ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Baadhi ya wafanyakazi benki ya Exim tawi la Shinyanga wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bi Sarah Tito (katikati) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans kilichopo Mkoani Shinyanga mara baada ya kukabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Baadhi ya wafanyakazi benki ya Exim tawi la Karatu wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bw John Ndyebonera (katikati) wakifurahia pamoja na watoto na uongozi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Shalom Orphanage and Children Care Centre cha Wilayani Karatu wakati wakabidhi msaada wa chakula ili kuwawezesha watoto hao waweze kufurahia Sikukuu ya Eid-Ul-Fitr kama watoto wengine waliopo majumbani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...